Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 23 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 23 Oktoba 2027

Jumamosi · Juma la 29 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 29 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Yohane wa Kapistrano, padre · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Rum 8:1–11

1Kwa hiyo basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. 2Kwa kuwa kanuni ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imenifanya mimi kuwa huru mbali na kanuni ya dhambi na mauti. 3Kwa maana kile ambacho sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ilikuwa dhaifu katika mwili, Mungu alifanya. Alimtuma Mwana wake wa pekee kwa mfano wa mwili wa dhambi awe sadaka ya dhambi, na akaihukumu dhambi katika mwili. 4Alifanya hivi ili maagizo ya sheria yatimilizwe ndani yetu, sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali kwa kufuata mambo ya Roho. 5Wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, lakini wale waifuatao Roho huyafikiri mambo ya Roho. 6Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya Roho ni uzima na amani. 7Hii ni kwa sababu ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 8Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. 9Hata hivyo, hampo katika mwili bali katika Roho, kama ni kweli kwamba Roho wa Mungu huishi ndani yenu. Lakini kama mtu hana Roho wa Kristo, yeye si wake. 10Kama Kristo yumo ndani yenu, mwili umekufa kwa mambo ya dhambi, bali roho ni hai kwa mambo ya haki. 11Ikiwa Roho wa yule aliyemfufua Yesu kutoka wafu huishi ndani yenu, yeye yule aliyemfufua Kristo kutoka katika wafu ataipa pia miili yenu ya mauti uhai kwa njia ya Roho wake, aishie ndani yenu.

Wimbo wa katikati

Zab 24:1–6

1Zaburi ya Daudi. Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake. 2Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito. 3Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake? 4Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya. 5Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake. 6Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo.

Injili

Lk 13:1–9

1Kwa wakataihuo huo, kulikuwa na baadhi watu waliomtaarifu juu ya Wagalilaya ambao Pilato aliwaua na kuchanganya damu yao na sadaka zao. 2Yesu akajibu na kuwaambia, “Je mwadhani kuwa Wagalilaya hao walikuwa na dhambi kuliko Wagalilaya wengine wote ndiyo maana wamepatwa na mabaya hayo? 3Hapana, nawaambia, lakini msipotubu, nanyi mtaangamia vivyo hivyo. 4Au wale watu kumi na nane katika Siloamu ambao mnara ulianguka na kuwaua, mnafikiri wao walikuwa wenye dhambi zaidi kuliko watu wengine katika Yerusalemu? 5Hapana, mimi nasema, lakini kama msipotubu, ninyi nyote pia mtaangamia. 6Yesu aliwaambia mfano huu, “Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake na alikwenda kutafuta matunda juu yake lakini hakupata. 7Akamwambia mtunza bustani, 'Tazama, kwa miaka mitatu nimekuja na kujaribu kutafuta matunda kwenye mtini huu lakini sikupata. Uukate. Kwani ulete uharibifu wa ardhi? 8Mtunza bustani akajibu na kusema, 'uache mwaka huu ili niupalilie na kuweka mbolea juu yake. 9Kama ukizaa matunda mwaka ujao, ni vema; lakini kama hautazaa, uukate.!”'

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 23 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki