Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 22 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 22 Oktoba 2027
Ijumaa · Juma la 29 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Ijumaa ya Juma la 29 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Yohane Paulo II, papa · Kumbukumbu ya hiari
Kufunga na toba
Siku ya toba
Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.
Masomo ya siku
Somo la kwanza
18Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai jambo jema. Kwa kuwa tamaa ya lililo jema imo ndani yangu, lakini silitendi. 19Kwa maana lile jema nilipendalo silitendi, bali lile ovu nisilolipenda ndilo nilitendalo. 20Sasa kama natenda lile nisilolipenda, si mimi binafsi nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 21Nimefahama, tena, imo kanuni ndani yangu ya kutaka kutenda lililo jema, lakini uovu hakika umo ndani yangu. 22Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani. 23Lakini naona kanuni iliyo tofauti katika viungo vya mwili wangu. Inapiga vita dhidi ya kanuni mpya katika akili zangu. Inanifanya mimi mateka kwa kanuni ya dhambi iliyo katika viungo vya mwili wangu. 24Mimi ni mtu wa huzuni! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? 25Lakini shukrani kwa Mungu kwa Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo basi. Mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu. Bali, kwa mwili naitumikia kanuni ya dhambi.
Wimbo wa katikati
66Unifundishe utambuzi sahihi na uelewa, kwa kuwa nimeamini katika amri zako. 68Wewe ni mwema, na ndiye yule utendaye mema; unifundishe sheria zako. 76Agano lako aminifu na linifariji, kama ulivyomwahidi mtumishi wako. 77Unihurumie ili niweze kuishi, kwa maana sheria yako ni furaha yangu. 93Sitayasahau kamwe maagizo yako, maana kupitia hayo umeniweka hai. 94Mimi ni wako, kwa maana ninayatafuta maagizo yao.
Injili
54Yesu akawa anawaambia makutano pia, “Mara muonapo mawingu yakitokea magharibi, mnasema nyakati za mvua zimewadia; na ndivyo inavyo kuwa, 55Na upepo wa kusini ukivuma, mnasema, Patakuwepo na joto kali, na ndivyo inavyokuwa. 56Enyi wanafiki, mnaweza kutafsiri mwonekano wa nchi na anga, lakini inakuwaje hamuwezi kuutafsiri wakati uliopo? 57Ni kwa nini kila mmoja wenu asipambanue lililo sahihi kwake kulifanya wakati ambapo angali na nafasi ya kufanya hivyo? 58Maana mkienda na mshitaki wako mbele ya hakimu, jitahidi kupatana na mshitaki wako mungali bado mko njiani asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akupeleka kwa ofisa, na ofisa akakutupa gerezani. 59Nakuambia, hutatoka huko hadi umelipa mpaka senti ya mwisho.
Watakatifu wa siku
- Mt. Yohane Paulo II, papa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki