Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 18 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 5 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 18 Oktoba 2027
Jumatatu · Wiki ya 18 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Mfiadini Kharitina (304)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
25Kwa hiyo, weka mbali udanganyifu. “Ongeeni ukweli, kila mmoja na jirani yake,” kwa sababu tu washirika kwa kila mmoja kwa mwenzake. 26Mwe na hasira, lakini msitende dhambi.” Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu. 27Msimpe Ibilisi nafasi. 28Yeyote aibaye lazima asiibe tena. Badala yake ni lazima afanye kazi. Afanye kazi yenye manufaa kwa mikono yake, ili kwamba aweze kumhudumia mtu aliye na hitaji. 29Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu. Badala yake, maneno lazima yatoke katika vinywa vyenu yafaayo kwa mahitaji, kuwapa faida wale wanaosikiliza. 30Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu. Ni kwa Yeye kwamba mmewekewa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi. 31Lazima muweke mbali uchungu wote, ghadhabu, hasira, ugomvi, na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wema ninyi kwa ninyi. 32Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Injili
24Lakini ole wenu mlio matajiri! Kwa maana mmekwisha pata faraja yenu. 25Ole wenu mlio shiba sasa! Kwa maana mtaona njaa baadaye. Ole wenu mnaocheka sasa! Kwa maana mtaomboleza na kulia baadaye. 26Ole wenu, mtakaposifiwa na watu wote! Kwa maana baba zao waliwatendea manabii wa uongo vivyohivyo. 27Lakini nasema kwenu ninyi mnaonisikiliza, wapendeni adui zenu na kufanya mema kwa wanao wachukieni. 28Wabarikini wale wanao walaani ninyi na waombeeni wale wanaowaonea. 29Kwake yeye akupigaye shavu moja, mgeuzie na la pili. Kama mtu akikunyang'anya joho lako usimzuilie na kanzu. 30Mpe kila akuombaye. Kama mtu akikunyang'anya kitu ambacho ni mali yako, usimuombe akurudishie.
Watakatifu wa siku
- Maaskofu Watakatifu Petro, Aleksi, Yona, Makario, Filipo, Ayubu, Hermogeni, Tikhon, Petro, Filareti, Inokenti na Makario, watenda miujiza wa Moscow na Urusi yote
- Mtakatifu Mtawa Gabrieli Mwungamaji (1959)
- Mfiadini wa Kikasisi Dionisio, Askofu wa Aleksandria (264-265)
- Mfiadini Mamelkhva wa Uajemi (karibu 344)
- Mtakatifu Mtawa Gregori wa Khandzta (861)
- Watakatifu Watawa wa Mapango ya Kyiv: Damiani, padri, mponyaji (1071), Yeremia (karibu 1070) na Mathayo (karibu 1085), wenye kuona mbali
- Mtakatifu Mtawa Kharitina, binti wa mfalme wa Lithuania, aliyejitahidi huko Novgorod (1281)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 5 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 18 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki