Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 18 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 18 Oktoba 2027

Jumatatu · Juma la 29 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Mt. Luka, mwinjili

Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyekundu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

2 Tim 4:9–17

9Jitahidi kuja kwagu haraka. 10Kwa kuwa Dema ameniacha. Anaupenda ulimwengu wa sasa na amekwenda Thesalonike, Kreseni alikwenda Galatia, na Tito alikwenda Dalmatia. 11Luka tu ndiye yuko pamoja nami. Umchukue Marko uje naye kwani yeye ni muhimu kwangu katika huduma. 12Nimemtuma Tikiko Efeso. 13Lile joho ambalo nililiacha Troa kwa Karpo, utakapokuja lilete, pamoja na vile vitabu hasa vile vya ngozi. 14Alekizanda mfua chuma alinitendea maovu mengi. Bwana atamlipa kulingana na matendo yake. 15Nawe pia jihadhari naye, kwani aliyapinga sana maneno yetu. 16Katika utetezi wangu wa kwanza, hakuna mtu yeyote aliyesimama pamoja nami, badala yake, kila mmoja aliniacha. Mungu asiwahesabie hatia. 17Lakini Bwana alisimama pamoja nami, akanitia nguvu ili kwamba kupitia kwangu, neno linenwe kwa ukamilifu na mataifa wapate kusikia. Niliokolewa katika kinywa cha Simba.

Wimbo wa katikati

Zab 145:10–13, 17–18

10Vyote ulivyo viumba vitakushukuru wewe, Yahwe; waaminifu wako watakutukuza wewe. 11Waaminifu wako watanena juu ya utukufu wa ufalme wako, na watahubiri juu ya nguvu zako. 12Watayafanya matendo makuu ya Mungu ya julikane na wanadamu na utukufu wa fahari ya ufalme wake. 13Ufalme wako ni wa milele, na mamlaka yako ya dumu kizazi hata kizazi. 17Yahwe ni mwenye haki katika njia zake zote na neema katika yote afanyayo. 18Yahwe yu karibu na wote wamwitao, wale wamwitao yeye katika uaminifu.

Injili

Lk 10:1–9

1Baada ya mambo hayo, Bwana akachagua sabini wengine, na kuwatuma wawili wawili wamtangulie katika kila mji na eneo alilotarajia kwenda. 2Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache. Hivyo basi muombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume haraka wafanyakazi katika mavuno yake. 3Enendeni katika miji. Angalieni, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. 4Msibebe mfuko wa pesa, wala mikoba ya wasafiri, wala viatu, wala msimsalimie yeyote njiani. 5Katika nyumba yeyote mtakayo ingia, kwanza semeni, 'Amani iwe katika nyumba hii.' 6kama mtu wa amani yupo pale, amani yenu itabaki juu yake, lakini kama sivyo, itarudi kwenu. 7Bakini katika nyumba hiyo, kuleni na mnywe watakachokitoa, kwa maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msihame kutoka nyumba hii kwenda nyingine. 8Mji wowote muuingiao, na wakawapokea, kuleni chochote kitakachowekwa mbele yenu, 9na ponyeni wagonjwa waliomo humo. Semeni kwao, 'Ufalme wa Mungu umekuja karibu yanu'

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 18 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki