Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 17 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 4 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 17 Oktoba 2027
Jumapili · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Jumapili ya 17 baada ya Pentekoste
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Injili ya 6 ya Sala ya Alfajiri
36Wakati wakiongea mambo hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akawaambia, “Amani iwe kwenu.” 37Lakini waliogopa na kujawa na hofu, na wakafikiri kwamba waliona roho. 38Yesu akawaambia, Kwanini mnafadhaika? Kwanini maswali yanainuka mioyoni mwenu? 39Angalieni mikono yangu na miguu yangu, kwamba ni mimi mwenyewe. Niguseni na muone. Kwa maana roho haina nyama na mifupa, kama mnionavyo mimi kuwa navyo.” 40Alipokwisha kusema hivi, akawaonyesha mikono yake na miguu yake. 41Walipokuwa bado na furaha iliyochanganyikana na kutokuamini, na kustaajabu, Yesu akawaambia, “Je mna kitu chochote cha kula?” 42Wakampa kipande cha samaki aliyechomwa. 43Yesu akakichukua, na kukila mbele yao. 44Akawaambia, “Nilipokuwa nanyi, niliwaambia kwamba yote yalioandikwa kwenye sheria ya Musa na manabii na Zaburi lazima yatimilike.” 45Kisha akafungua akili zao, kwamba waweze kuyaelewa maandiko. 46Akawaambia, “Kwamba imeandikwa, Kristo lazima ateseke, na kufufuka tena kutoka katika wafu siku ya tatu. 47Na toba na msamaha wa dhambi lazima ihubiriwe kwa jina lake kwa mataifa yote, kuanzia kutokea Yerusalemu. 48Ninyi ni mashahidi wa mambo haya. 49Angalia, nawapelekea ahadi ya Baba yangu juu yenu. Lakini subirini hapa jijini, mpaka mtakapovishwa nguvu kutoka juu. 50Kisha Yesu akawaongoza nje mpaka walipokaribia Bethania. Akainua mikono yake juu, na akawabariki. 51Ikatokea kwamba, wakati alipokuwa akiwabariki, aliwaacha na akabebwa juu kuelekea mbinguni. 52Basi wakamwabudu, na kurudi Yerusalemu na furaha kuu. 53Waliendelea kuwepo hekaluni, wakimbariki Mungu.
Waraka
16Na kuna makubaliano gani yapo kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai, kama ambavyo Mungu alisema: “Nitakaa kati yao na kutembea kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.” 17Kwa hiyo, “Tokeni kati yao, na mkatengwe nao,” asema Bwana. “Msiguse kitu kichafu, na nitawakaribisha ninyi. 18Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa wanangu wa kiume na wa kike,” asema Bwana Mwenyezi. 7:1Wapendwa wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizi, na tujitakase wenyewe kwa kila jambo ambalo linatufanya kuwa wachafu katika miili yetu na katika roho. Na tuutafute utakatifu katika hofu ya Mungu.
Injili
31Kama mpendavyo watu wawatendee, nanyi watendeeni vivyo hivyo. 32Kama mkiwapenda watu wawapendao ninyi tu, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwamaana hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao. 33Kama mkiwatendea mema wale wanaowatendea ninyi mema, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwa maana hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. 34Kama mkikopesha vitu kwa watu ambao mnategemea watawarudishia, hiyo ni thawabu gani kwenu? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, na hutegemea kupokea kiasi hicho hicho tena. 35Lakini wapendeni adui zenu na watendeeni mema. Wakopesheni na msihofu kuhusu kurudishiwa, na thawabu yenu itakuwa kubwa. Mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwasababu yeye mwenyewe ni mwema kwa watu wasio na shukurani na waovu. 36Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Hierotheo, Askofu wa Athene (karne ya 1)
- Kupatikana kwa masalia ya Maaskofu Watakatifu Guri, Askofu Mkuu wa Kazan, na Barsanufio, Askofu wa Tver (1595)
- Mfiadini wa Kikasisi Demetrio, padri (1918)
- Wafiadini wa Kikasisi Nikolao, Mikaeli, Yakobo na Tikhon, mapadri, Mtawa Mfiadini Basili (1937)
- Mtakatifu Khionia Mwungamaji (1945)
- Wafiadini Gayo, Fausto, Eusebio na Kheremoni (karne ya 3)
- Mfiadini wa Kikasisi Petro wa Kapitolia (karne ya 3-4)
- Wafiadini Domnina na binti zake Virinea (Veronika) na Proskudia (Prosdoka) (305-306)
- Mfiadini Dabikto (Adavkto) (karibu 305-313)
- Mtakatifu Mtawa Amoni (karibu 350)
- Mtakatifu Mtawa Paulo Mwenye Moyo Mnyofu (karne ya 4)
- Mwana wa Mfalme Mwaminifu Vladimir Yaroslavich wa Novgorod, mtenda miujiza (1052)
- Watakatifu Watawa Heladio na Onesimo wa Mapango ya Kyiv (karne ya 12-13)
- Mtakatifu Mtawa Amoni, mtawa wa faragha wa Mapango ya Kyiv (karne ya 13)
- Mwenye Haki Stefano Štiljanović (1515)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 4 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 17 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki