Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 17 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 17 Oktoba 2027
Jumapili · Juma la 29 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 29 ya Mwaka
Dominika · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
10Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Yahwe kumponda yeye na kumfanya yeye apone. Alipoyafanya maisha yake kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi, ataona watoto wake, ataongeza siku zao, na mapenzi ya Yahwe yatatimizwa kupitia yeye. 11Baada ya mateso ya maisha yake, ataona mwanga na ataridhika kwa maarifa yake.
Wimbo wa katikati
4Kwa kuwa maneno ya Mungu ni ya hakika, na kila afanyacho ni haki. 5Yeye hupenda haki na kutenda kwa haki. Dunia imejaa uaminifu wa agano la Yahwe. 18Tazama, macho ya Yahwe yako kwa wale wanao mhofu yeye, wale wanao litumainia agano lake takatifu 19kuwaokoa maisha yao na mauti na kuwaweka hai wakati wa jaa. 20Sisi tunamngoja Yahwe, yeye ni msaada wetu na ngao yetu. 22Yahwe, agano lako takatifu, liwe pamoja nasi tuwekapo tumaini letu katika wewe.
Somo la pili
14Baadaye kuwa na kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu Mwana wa Mungu, kwa uimara tushikilie imani zetu. 15Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu ambaye hawezi kuhisi huruma kwa ajili udhaifu wetu, lakini yeye ambaye kwa njia zote amekuwa akijaribiwa kama sisi, isipokuwa yeye ambaye hana dhambi. 16Na tuje kwa ujasiri katika kiti cha enzi cha neema, ili kwamba tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa hitaji.
Injili
35Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walikuja kwake na kusema, “Mwalimu, tunakuhitaji utufanyie chochote tukuombacho.” 36Aliwaambia, “Mnataka niwatendee nini?” 37Wakasema, “Turuhusu tukae nawe katika utukufu wako, mmoja katika mkono wako wa kuume na mwingine mkono wako wa kushoto.” 38Lakini Yesu aliwajibu, “Hamjui mnachoomba. Mnaweza kukinywea kikombe ambacho nitakiywea au kustahimili ubatizo ambao nitabatizwa?” 39Wakamwambia, “Tunaweza” Yesu akawaambia, “Kikombe nitakachokinywea, mtakinywea. Na ubatizo ambao kwao nimebatizwa, mtaustahimili. 40Lakini atakayekaa mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto sio mimi wa kutoa, lakini ni kwa wale ambao kwao imekwisha andaliwa.” 41Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana. 42Yesu akawaita kwake na kusema, “Mnajua kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala, na watu wao mashuhuri huwaonyesha mamlaka juu yao.” 43Lakini haipaswi kuwa hivi kati yenu. Yeyote atakaye kuwa mkubwa kati yenu lazima awatumikie, 44na yeyote atakaye kuwa wa kwanza kati yenu ni lazima awe mtumwa wa wote. 45Kwa kuwa Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kuyatoa maisha yake kuwa fidia kwa wengi.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Ignasi wa Antiokia, askofu na shahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki