Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 28 Septemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 28 Septemba 2027

Jumanne · Juma la 26 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumanne ya Juma la 26 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Wenselaus, shahidi · Kumbukumbu ya hiari

Watakatifu Laurenti Ruiz na wenzake, mashahidi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Zek 8:20–23

20Yahwe wa majeshi asema hivi: Watu watakuja tena, hata wanaoishi miji mingine. 21Watu wa mji mmoja watakwenda mji mwingine na kusema, “Haya twendeni haraka mbele ya Yahwe tukaombe na kumtafuta Yahwe wa majeshi! Sisi wenyewe tunakwenda pia. 22Watu wengi na mataifa yenye nguvu yatakuja kumtafuta Yahwe wa majeshi huko Yerusalemu na kuomba upendeleo kwa Yahwe! 23Yahwe wa majeshi asema hivi: Katika siku hizo watu kumi kutoka katika kila lugha na taifa watashika upindo wa kanzu zenu na kusema, “Haya sisi nasi tutakwenda pamoja nanyi, kwani tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nayi!”

Wimbo wa katikati

Zab 87:1–7

1Zaburi ya wana wa Kora; wimbo. Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu; 2Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo. 3Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. Selah 4Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'” 5Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha. 6Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” Selah 7Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”

Injili

Lk 9:51–56

51Ikatokea kwamba, kulinga na siku zilivyokua zikikaribia zsiku zake za kwenda mbinguni, kwa uimara alielekeza uso wake Yerusalemu. 52Akatuma wajumbe mbele yake, nao wakaenda na kuingia katika kijiji cha Wasamaria ili wamtayarishie mahali. 53Lakini watu huko hawakumpokea, kwasababu alikua ameelekeza uso wake Yerusalemu. 54Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipo liona hili, wakasema, “Bwana unahitaji tuamuru moto ushuke chini kutoka mbinguni uwateketeze?” 55Lakini aliwageukia akawakemea. 56Kisha walikwenda kijiji kingine.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 28 Septemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki