Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 27 Septemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 27 Septemba 2027
Jumatatu · Juma la 26 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 26 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Vinsenti wa Paulo, padre · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Neno la Yahwe wa majeshi likanijia kusema, 2“Yahwe wa majeshi asema hivi: Nina huzuni kwa ajili ya Sayuni kwa wivu mkuu na ninamaumivu kwa hasira nyingi! 3Yahwe wa majeshi asema hivi: Nitairudia Sayuni nami nitakaa kati ya Yerusalemu, kwa kuwa Yerusalemu itaitwa mji wa kweli na mlima wa Yahwe wa majeshi utaitwa Mlima Mtakatifu! 4Yahwe wa majeshi asema hivi: Kwa mara nyingine tena kutakuwa na vikongwe katika mitaa ya Yerusalemu, na kila mtu ataitaji mkongojo mkononi mwake kwa vile alivyo mzee. 5Pia mitaa ya mji itajazwa na vijana wa kiume na kike wachezao. 6Yahwe wa majeshi asema hivi: ikiwa jambo laonekana haliwezekani katika macho ya masalia ya watu hawa katika siku hizo, je haliwezekani pia machoni pangu? - asema Yahwe. 7Yahwe wa majeshi asema hivi: Tazama, nipo tayari kuwaokoa watu wangu kutoka nchi ya mawio na ya machweo ya jua! 8Kwa maana nitawarudisha tena, nao wataishi ndani ya Yerusalemu, hivyo watakuwa watu wangu tena, nami nitakuwa Mungu wao katika kweli na utakatifu!
Wimbo wa katikati
15Mataifa wataliheshimu jina lako, Yahwe, na wafalme wote wa nchi watauheshimu utukufu wako. 16Yahwe ataijenga tena Sayuni na ataonekana katika utukufu wake. 17Wakati huo, atajibu maombi ya fukara; hatayakataa maombi yao. 18Hii itaandikwa kwa ajili ya vizazi vijavyo, na watu ambao bado hawajazaliwa watamsifu Yahwe. 19Maana ametazama chini toka mahali pa juu patakatifu; 20Toka mbinguni Yahwe ameiangalia nchi, ili kusikia kuugua kwa wafungwa, kuwafungua waliohukumiwa kufa. 28Watoto wa watumishi wako wataendelea kuishi, na uzao wao utaishi katika uwepo wako. 21Kisha watu watalitangaza jina la Yahwe katika Sayuni na sifa zake katika Yerusalemu 22pindi mataifa na falme watakapokusanyika pamoja kumtumikia Yahwe.
Injili
46Kisha mgogoro ulianza ulizuka miongoni mwao i juu ya nani angekuwa mkuu. 47Lakini Yesu alipotambua walichokuwa wakihojiana mioyoni mwao, alimchukua mtoto mdogo, na kumuweka upande wake, 48na akasema, “ kama mtu yeyote akimpokea mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, anipokea mimi pia, na yeyote akinipokea mimi, ampokea pia aliyenituma, kwa kuwa aliye mdogo kati yenu wote ndiye alie mkuu” 49Yohana akajibu akasema, “Bwana, tulimuona mtu akifukuza pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu haambatani na sisi.” 50Lakini Yesu akamwambia, “Msimzuie, kwa kuwa asiye kinyume na ninyi ni wa kwenu”
Watakatifu wa siku
- Mt. Vinsenti wa Paulo, padre
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki