Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 11 Septemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 29 Agosti (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 11 Septemba 2027

Jumamosi · Wiki ya 12 baada ya Pentekoste · Sauti ya 2

Sikukuu na watakatifu

Kukatwa kichwa kwa Nabii Yohana, Mtangulizi na Mbatizaji wa Bwana

Mfungo wa siku moja · Mfungo mkali

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Sala ya Jioni: somo

Isa 40; Isa 41; Isa 45; Isa 48; Isa 54 (mistari iliyochaguliwa)

Sala ya Jioni: somo

Mal 3; Mal 4 (mistari iliyochaguliwa)

Sala ya Jioni: somo

Haimo katika tafsiri hii

Sala ya Alfajiri: Injili

Mt 14:1–13

1Kwa wakati huo, Herode alisikia habari juu ya Yesu.. 2Akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka katika wafu. Kwa hiyo nguvu hizi zipo juu yake.” 3Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake. 4Kwa kuwa Yohana alimwambia, “Si halali kumchukua yeye kuwa mke wake.” 5Herode angemwua lakini aliwaogopa watu kwa sababu walimwona Yohana kuwa nabii. 6Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode. 7Katika kujibu kili aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba. 8Baada ya kushauriwa na mama yake, alisema, “Nipe mimi hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.” 9Mfalme alikuwa na sikitiko kwa maombi ya binti, lakini kwa ajili ya kiapo chake, kwa sababu ya wote waliokuwa chakulani pamoja naye aliamuru kwamba inapaswa ifanyike. 10Alituma Yohana aletwe kutoka gerezani 11ili akatwe kichwa chake na kikaletwa juu ya sinia na akapewa binti na akakipeleka kwa mama yake. 12Kisha wanafunzi wake wakaja kuuchukua ule mwili na kuuzika, baada ya hili walienda kumwambia Yesu. 13Naye Yesu aliposika haya, akijatenga kutoka mahali pale akapanda ndani ya mashuka akaenda sehemu iliyotengwa. Wakati umati ulipo fahamu alikokuwa, walimfuata kwa miguu kutoka mijini.

Waraka (Mtangulizi)

Mdo 13:25–32

25Naye Yohana alipokuwa akimalizia kazi yake, alisema, 'Mwanifikiri mimi ni nani? mimi si yule. Lakini sikilizeni, ajaye nyuma yangu, sisitahili kulegeza viatu vya miguu yake.' 26Ndugu, watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wale ambao kati yenu mnamwabudu Mungu, ni kwa ajili yetu kwamba ujumbe huu wa ukombozi umetumwa. 27Kwa wale waishio Yerusalemu, na watawala wao, hawakumtambua kwa uhalisia, na wala hawakuutambua ujumbe wa manabii ambao husomwa kila Sabato; kwa hiyo walitimiliza ujumbe wa manabii kwa kumhukumu kifo Yesu. 28Japokuwa hawakupata sababu nzuri kwa kifo ndani yake, walimwomba Pilato amuue. 29Walipomaliza mambo yote yaliyoandikwa kuhusu yeye, walimshusha kutoka mtini na kumlaza kaburini. 30Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu. 31Alionekana kwa siku nyingi kwa wale waliokwenda pamoja naye kutoka Galilaya kuelekea Yerusalemu. Watu hawa sasa ni mashahidi wa watu. 32Hivyo tunawaletea habari njema kuhusu ahadi walizopewa mababu zetu.

Injili (Mtangulizi)

Mk 6:14–30

14Mfalme Herode aliposikia hayo, kwa kuwa jina la Yesu lilikuwa limejulikana sana. Baadhi walisema, “Yohana mbatizaji amefufuka na kwa sababu hiyo, hii nguvu ya miujiza inafanya kazi ndani yake.” 15Baadhi yao wakasema, “Huyu ni Eliya,” Bado wengine wakasema, “Huyu ni nabii, kama mmoja wa wale manabii wa zamani.” 16Lakini Herode aliposikia haya akasema, “Yohana, niliyemkata kichwa amefufuliwa.” 17Maana Herode mwenyewe aliagiza Yohana akamatwe na alimfunga gerezani kwa sababu ya Herodia (mke wa kaka yake Filipo) kwa sababu yeye alikuwa amemuoa. 18Kwa maana Yohana alimwambia Herode, “Si halali kumuoa mke wa kaka yako.” 19Lakini Herodia alianza kumchukia na alikuwa akitaka kumuua, lakini hakuweza, 20maana Herode alimwogopa Yohana; alijua kwamba ni mwenye haki mtu mtakatifu, na alimwacha salama. Na alipoendelea kumsikiliza alihuzunika sana, lakini alifurahi kumsikiliza. 21Hata ilipofika wakati mwafaka ikiwa imekaribia siku ya kuzaliwa Herode akawaandalia moafisa wake karamu, na makamanda, na viongozi wa Galilaya. 22Ndipo binti wa Herodia akaingia na kucheza mbele yao, akamfurahisha Herode na wageni walioketi wakati wa chakula cha jioni. Ndipo mfalme akamwambia binti, “Niombe chochote unachotaka nami nitakupa.” 23Akamwapia na kusema, chochote utakachoniomba, nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu.” 24Akatoka nje akamuuliza mama yake, “Niombe nini?” Akasema, “Kichwa cha Yohana Mbatizaji.” 25Na mara moja akaingia kwa mfalme akaanza kusema, “Nataka unipatie ndani ya sahani, kichwa cha Yohana Mbatizaji.” 26Mfalme alisikitishwa sana, lakini kwa sababu ya kiapo chake na kwa ajili ya wageni, hakuweza kumkatalia ombi lake. 27Hivyo, mfalme akatuma askari kati ya walinzi wake na kuwaagiza kwenda kumletea kichwa cha Yohana. Mlinzi alikwenda kumkata kichwa akiwa kifungoni. 28Akakileta kichwa chake kwenye sahani na kumpatia binti, na binti akampa mama yake. 29Na wanafunzi wake waliposikia hayo, walikwenda kuuchukua mwili wake wakaenda kuuzika kaburini. 30Na mitume, walikusanyika pamoja mbele ya Yesu, wakamweleza yote waliyofanya na waliyoyafundisha.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 11 Septemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 29 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 11 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki