Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 11 Septemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 11 Septemba 2027
Jumamosi · Juma la 23 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 23 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Kumbukumbu ya Bikira Maria siku ya Jumamosi · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
15Ujumbe huu ni wa kuaminika na unastahili kupokelewa na wote, ya kuwa Kristo Yesu alikuja duniani kuokoa wenye dhambi. Mimi ni mbaya zaidi ya wote. 16Lakini kwa sababu hii mimi nilipewa rehema ili kwamba ndani yangu mimi, awali ya yote, Kristo Yesu adhihirishe uvumilivu wote. Alifanya hivyo kama kielelezo kwa wote watakaomtumaini Yeye kwa ajili ya uzima wa milele. 17Na sasa kwa Mfalme asiye na ukomo, asiyekufa, asiyeonekana, Mungu pekee, iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.
Wimbo wa katikati
1Msifuni Yahwe. Msifuni yeye, enyi watumishi wa Yahwe; lisifuni jina la Yahwe. 2Litukuzwe jina la Yahwe, tangu sasa na hata milele. 3Toka maawio ya jua hata machweo yake, Jina la Yahwe lazima lisifiwe. 4Yahwe ameinuliwa juu ya mataifa yote, na utukufu wake wafika juu mbinguni. 5Ni nani aliye kama Yahwe Mungu wetu, aliye na kiti chake juu, 6atazamaye chini angani na duniani? 7Humwinua maskini toka mavumbini na kumpandisha muhitaji kutoka jaani,
Injili
43Kwa sababu hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri. 44Kwa sababu kila mti hutambulika kwa matunda yake. Kwa sababu watu hawachumi tini kutoka kwenye miba, wala hawachumi zabibu kutoka kwenye michongoma. 45Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu. Kwa sababu kinywa chake husema yale yaujazayo moyo wake. 46Kwanini mnaniita, 'Bwana, Bwana', na bado hamyatendi yale nisemayo? 47Kila mtu ajaye kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatendea kazi, nitawaonyesha jinsi alivyo. 48Anafanana na mtu ajengae nyumba yake, ambaye huchimba chini sana, na kujenga msingi wa nyumba juu ya mwamba imara. Mafuriko yalipokuja, maporomoko ya maji yaliipiga nyumba, lakini hayakuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri. 49Lakini yeyote asikiaye neno langu na hakulitii; mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ulipoishukia kwa nguvu, nyumba ile ilitopata maangamizi makubwa.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki