Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 10 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 28 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 10 Septemba 2027
Ijumaa · Wiki ya 12 baada ya Pentekoste · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Musa Mweusi (karibu 400)
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Sala ya Jioni: somo
Haimo katika tafsiri hii
Sala ya Jioni: somo
Haimo katika tafsiri hii
Sala ya Jioni: somo
Haimo katika tafsiri hii
Sala ya Alfajiri: Injili
27Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia. 28Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. 29Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. 30Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
Waraka
10Kwa kuwa huzuni ya kiungu huleta toba ambayo hukamilisha wokovu bila ya kuwa na majuto. Huzuni ya kidunia, hata hivyo, huleta mauti. 11Angalieni huzuni hii ya kiungu ilizalisha azma gani kubwa ndani yenu. Jinsi gani azma ilikuwa kubwa ndani yenu kuthibitisha kuwa hamkuwa na hatia. Kwa jinsi gani uchungu wenu ulivyokuwa mkubwa, hofu yenu, matamanio yenu, bidii yenu, na shauku yenu kuona kwamba haki inapaswa kutendeka! Katika kila jambo mmethibitisha wenyewe kutokuwa na hatia. 12Ingawa niliwaandikia ninyi, sikuandika kwa ajili ya mkosaji, wala si kwa mtu aliyeteswa na maovu. Nimeandika ili kwamba udhati wa mioyo yenu kwa ajili yetu ifanywe kujulikana kwenu mbele ya macho ya Mungu. 13Ni kwa ajili ya hii kwamba tunafarijika. Katika nyongeza ya faraja yetu wenyewe, tunafurahi pia, hata zaidi kwa sababu ya furaha ya Tito, kwa kuwa roho yake iliburudishwa na ninyi nyote. 14Kwa kuwa kama nilijivuna kwake kuhusiana na ninyi, sikuwa na aibu. Kinyume chake, kama tu kila neno tulilolisema kwenu lilikuwa kweli, Majivuno yetu kuhusu ninyi kwa Tito yalithibitisha kuwa kweli. 15Upendo wake kwa ajili yenu hata ni mkubwa zaidi, kama akumbukapo utii wenu nyote, jinsi mlivyomkaribisha yeye kwa hofu na kutetemeka. 16Ninafurahi kwa sababu nina ujasiri kamili ndani yenu.
Waraka (ya Jumamosi)
26Angalia wito wa Mungu juu yenu, kaka na dada zangu. Si wengi wenu mlikuwa na hekima katika viwango vya kibinadamu. Si wengi wenu mlikuwa na nguvu. Si wengi wenu mlizaliwa katika ukuu. 27Lakini Mungu alichagua vitu vijinga vya dunia ili kuviaibisha vyenye hekima. Mungu alichagua kilicho dhaifu katika dunia kukiaibisha chenye nguvu. 28Mungu alichagua kile kilicho cha hali ya chini na kilichodharauliwa katika dunia. Alichagua hata vitu ambavyo havikuhesabiwa kuwa kitu, kwa kuvifanya si kitu vitu vilivyo na thamani. 29Alifanya hivi ili asiwepo yeyote aliye na sababu ya kujivuna mbele zake.
Waraka (Mt. Ayubu)
22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani, 23upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo. 24Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya. 25Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho. 26Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu. 6:1Ndugu, ikiwa mtu amekamatwa katika uovu, ninyi mlio wa kiroho, mnawiwa kumrejesha huyo ndugu katika roho ya upole. Huku mkijiangalia wenyewe ili msijaribiwe. 2Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.
Injili
18Wanafunzi wa Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Na baadhi ya watu walikuja kwake na kumwambia, “Kwa nini wanafunzi wa Yohana na mafarisayo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi? 19Yesu aliwaambia, “Je waliohudhuria harusini wanaweza kufunga wakati bwana harusi bado akiwa pamoja nao? Kwa vyovyote bwana harusi akiwa bado yuko pamoja nao hawawezi kufunga.” 20Lakini siku zitakuja wakati bwana harusi atakapoondolewa kwao, na katika siku hizo wao watafunga. 21Hakuna mtu ashonaye kipande kipya cha nguo kwenye vazi kuukuu, vinginevyo kiraka kitabanduka kutoka katika hilo, kipya kubanduka kutoka katika kikuukuu, na kutakuwepo mpasuko mbaya. 22Hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu, vinginevyo divai itavipasua viriba na vyote viwili divai na viriba vitapotea. Badala yake, weka divai mpya katika viriba vipya.”
Injili (ya Jumamosi)
29Wakati wakitoka Yeriko, umati mkubwa ulimfuata. 30Na waliwaona vipofu wawili wameketi kando ya barabara. Waliposikia kuwa Yesu alikuwa anapita, walipaza sauti na kusema, “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie.” 31Lakini umati ukawakemea, na kuwaambia nyamazeni. Hata hivyo, wao wakapaza sauti zaidi na kusema, “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie.” 32Kisha Yesu alisimama na aliwaita na kuwauliza, “Mnataka niwafanyie nini?” 33Wakamwambia, “Bwana kwamba macho yetu yafumbuliwe.” 34Basi Yesu, akiwa amevutwa na huruma, akayagusa macho yao, mara hiyo, wakapokea uwezo wa kuona na wakamfuata.
Injili (Mt. Ayubu)
17Kisha Yesu alitelemka pamoja nao toka mlimani na kusimama mahali tambarare. Idadi kubwa ya wanafunzi wake walikuwa huko, pamoja na idadi kubwa ya watu kutoka Uyahudi na Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. 18Walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Watu waliokuwa wakisumbuliwa na pepo wachafu waliponywa pia. 19Kila mmoja kwenye hilo kusanyiko alijaribu kumgusa kwa sababu nguvu za uponyaji zilikuwa zikitokea ndani yake, na aliwaponya wote. 20Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu. 21Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka. 22Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu. 23Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Sava wa Krypetsk, wa Pskov (1495)
- Kupatikana kwa masalia ya Mtakatifu Mtawa Ayubu wa Pochaiv (1659)
- Mkutano wa Watakatifu Watawa Mababa wa Mapango ya Kyiv wanaopumzika katika Mapango ya Mbali (ya Mtakatifu Theodosio)
- Watawa Wafiadini wa Kazan Sergio, Laurenti, Serafim, Theodosio, Leontio, Stefano, Georgi, Hilarioni, Yohana na Sergio (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Nikolao, padri (1931)
- Mfiadini wa Kikasisi Basili, padri (1937)
- Mwenye Haki Ana nabii mke, binti wa Fanueli, aliyemlaki Bwana Yesu Kristo hekaluni Yerusalemu (karne ya 1)
- Mfiadini Shushanik, binti wa mfalme wa Rani (karne ya 5)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 28 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 10 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki