Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 12 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 30 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 12 Septemba 2027
Jumapili · Sauti ya 3
Sikukuu na watakatifu
Jumapili ya 12 baada ya Pentekoste
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Injili ya 1 ya Sala ya Alfajiri
16Lakini wale mitume kumi na mmoja walienda Galilaya, kwenye ule mlima aliokuwa amewaelekeza. 17Nao walipomwona, walimwabudu. lakini baadhi yao waliona shaka. 18Yesu akaja kwao akawambia akisema, “Nimepewa mamlaka yote duniani na mbinguni. 19Kwa hiyo enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Wabatizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtatkatifu. 20Wafundisheni kuyatii mambo yote niliyowaamuru, Na tazama, mimi niko pamoja nanyi daima, hata mpaka mwisho wa dunia.
Waraka
1Sasa ninawakumbusha, akina kaka na akina dada, juu ya injili niliyowahubiria, ambayo mliipokea na kusimama kwayo. 2Ni katika injili hii mmeokolewa, kama mkilishika imara neno nililowahubiri ninyi, isipokuwa mliamini bure. 3Kama kwanza nilivyo ipokea kwa umuhimu niliileta kwenu kama ilivyo: kwamba kutokana na maandiko, Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, 4kutokana na maandiko alizikwa, na kwamba alifufuka siku ya tatu. 5Na kwamba alimtokea Kefa, kisha kwa wale kumi na wawili. 6Kisha aliwatokea kwa wakati mmoja akina kaka na akina dada zaidi ya mia tano. Wengi wao bado wako hai, lakini baadhi yao wamelala usingizi. 7Kisha alimtokea Yakobo, kisha mitume wote. 8Mwisho wa yote, alinitokea mimi, kama vile kwa mtoto aliye zaliwa katika wakati usio sahihi. 9Kwa kuwa mimi ni mdogo kati ya mitume. Sistahili kuitwa mtume, kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu. 10Lakini kwa neema ya Mungu nipo kama nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Badala yake, nilifanya bidii kuliko wote. Lakini haikuwa mimi, bali neema ya Mungu iliyo ndani yangu. 11Kwa hiyo kama ni mimi au wao, tuna hubiri hivyo na tunaamini hivyo.
Injili
16Tazama mtu mmoja akaja kwa Yesu na kusema, “Mwalimu, ni kitu gani kizuri ninachotakiwa kufanya ili nipate kuwa na uzima wa milele?” 17Yesu akamwambia, “Kwa nini unaniuliza ni kitu gani kizuri? Kuna mmoja tu aliye mwema, lakini kama ukitaka kupata uzima, shika sheria za Mungu.” 18Yule mtu akamwuliza, “Ni sheria zipi?” Yesu akasema, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, 19waheshimu baba yako na mama yako, na mpende jirani yako kama nafsi yako.” 20Mtu yule akamwambia, “Mambo yote hayo nimeyatii. Bado ninahitaji nini? 21“Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze ulivyo navyo, na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo unifuate.” 22Lakini kijana yule aliposikia yale Yesu aliyomwambia, akaondoka kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na amemiliki mali nyingi. 23Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kweli nawaambieni, ni vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. 24Tena nawaambieni, ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” 25Wanafunzi waliposikia hivyo, wakashangaa sana na kusema, “Ni yupi basi atakayeokoka?” 26Yesu akawatazama na kusema, “Kwa wanadamu hilo haliwezekani, lakini kwa Mungu yote yanawezekana.”
Watakatifu wa siku
- Maaskofu Watakatifu Aleksanda (340), Yohana (595) na Paulo Mpya (784), Mapatriarki wa Konstantinopoli
- Mtakatifu Mtawa Aleksanda wa Svir (1533)
- Kuhamishwa kwa masalia ya Mwana wa Mfalme Mwaminifu Aleksanda Nevsky (1724)
- Kupatikana kwa masalia ya Mwana wa Mfalme Mwaminifu Danieli wa Moscow (1652)
- Mfiadini wa Kikasisi Petro, padri (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Paulo, padri, Mtawa Mfiadini Elisabeti na Mfiadini Theodoro (1937)
- Mtawa Mfiadini Ignatio (1938)
- Mtakatifu Petro Mwungamaji, padri (1972)
- Mtakatifu Mtawa Kristoforo Mroma (karne ya 6)
- Mtakatifu Mtawa Fantino, mtenda miujiza, huko Thesalonike (karne ya 9-10)
- Mkutano wa Maaskofu Watakatifu wa Serbia: Sava I (1237), Arsenio I (1266), Sava II (1269), Eustathio I (karibu 1285), Yakobo (1292), Nikodemo (1325), Danieli (1338), Maaskofu Wakuu; Yoanikio II (1354), Efraimu II (baada ya 1395), Spiridoni (1388), Makario (1574), Gabrieli I (1659), Mapatriarki, na Gregori, askofu
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 30 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 12 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki