Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 29 Agosti

Kalenda ya Kiorthodoksi · 16 Agosti (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 29 Agosti 2027

Jumapili · Sauti ya 1

Sikukuu na watakatifu

Jumapili ya 10 baada ya Pentekoste

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Injili ya 10 ya Sala ya Alfajiri

Yn 21:1–14

1Baada ya mambo hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi katika Bahari ya Tiberia; hivi ndivyo alivyojidhihirisha mwenyewe: 2Simon Petro alikuwa pamoja na Thomaso aitwaye Didimas, Nathanaeli wa kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili wa Yesu. 3Simon Petro akawaambia, “Mimi naenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Sisi, pia tutaenda nawe.” Wakaenda wakaingia kwenye mashua, lakini usiku huo wote hawakupata chochote. 4Na asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufukweni, nao wanafunzi hawakutambua kuwa alikuwa Yesu. 5Kisha Yesu akawambia, “Vijana, mna chochote cha kula?” Nao wakamjibu, “Hapana.” 6Akawambia, “Shusheni wavu upande wa kuume wa mashua, nanyi mtapata kiasi.” Kwa hiyo wakashusha wavu nao hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa cha samaki. 7Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akamwambia Petro, “Ni Bwana.” Naye Simon Petro aliposikia kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa vizuri), kisha akajitupa baharini. 8Wale wanafunzi wengine wakaja kwenye mashua (kwani hawakuwa mbali na pwani, yapata mita mia moja kutoka ufukweni), nao walikuwa wakivuta zile nyavu zilizokuwa zimejaa samaki. 9Walipofika ufukweni, waliona moto wa mkaa pale na juu yake kulikuwa na samaki pamoja na mkate. 10Yesu akawambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua sasa hivi.” 11Basi Simon Petro akapanda na kuukokota ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa, kiasi cha samaki 153; japo walikuwa wengi, ule wavu haukuchanika. 12Yesu akawaambia, “Njoni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanfunzi aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua kuwa alikuwa ni Bwana. 13Yesu akaja, akachukua ule mkate, kisha akawapa, akafanya vivyo hivyo na kwa wale samaki. 14Hii ilikuwa mara ya tatu kwa Yesu kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka toka wafu.

Waraka

1 Kor 4:9–16

9Kwa hiyo ninadhani Mungu ametuweka sisi mitume kama kutuonyesha wa mwisho katika mustari wa maandamano na kama watu waliohukumiwa kuuawa. Tumekuwa kama tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa wanadamu. 10Sisi ni wajinga kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye hekima katika Kristo. Tu wanyonge, lakini ninyi mna nguvu. Mnaheshimiwa, lakina sisi tunadharauliwa. 11Hata saa hii tuna njaa na kiu, hatuna nguo, tuna mapigo, na tena hatuna makazi. 12Tunafanya kazi kwa bidii, kwa mikono yetu wenyewe. Tunapodharauliwa, twabariki. Wakati tunapoteswa, twavumilia. 13Tunapotukanwa, twarudisha kwa upole. Tumekuwa, na tu bado tunahesabiwa kuwa kama kukataliwa na dunia na takataka kwa mambo yote. 14Siandiki mambo haya kuwaaibisha ninyi, lakini kuwarudi ninyi kama watoto wangu niwapendao. 15Hata kama mna waalimu makumi elfu katika Kristo, hamna baba wengi. Kwa kuwa nimekuwa baba yenu katika Yesu Kristo kupitia injili. 16Hivyo ninawasihi mniige mimi.

Waraka (Picha Isiyochorwa kwa Mikono)

Kol 1:12–18

12Tunaomba kwamba, kwa furaha, mtatoa shukrani kwa Baba, aliyewafanya ninyi mweze kuwa na sehemu katika urithi wa waumini katika nuru. 13Ametuokoa kutoka katika utawala wa giza na kutuhamishia katika ufalme wa Mwana wake mpendwa. 14Katika Mwanae tuna ukombozi, msamaha wa dhambi. 15Mwana ni mfano wa Mungu asiyeonekana. Ni mzaliwa wa kwanza wa uumbaji wote. 16Kwakuwa kwa yeye vitu vyote viliumbwa, vile vilivyoko mbinguni na vilivyoko duniani, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. ikiwa ni vya enzi au mamlaka au utawala au wenye nguvu, vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake. 17Yeye amekuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja. 18Na yeye ndiye kichwa cha mwili yaani kanisa, yeye ni mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka miongoni mwa wafu, hivyo, ana nafasi ya kwanza miongoni mwa vitu vyote.

Injili

Mt 17:14–23

14Walipofika katika umati wa watu, mtu mmoja alimwendea, akapiga magoti mbele zake, na kumwambia, 15“Bwana, umhurumie mwanangu, maana amekuwa na kifafa na kuteseka sana. Kwa kuwa mara nyingi huanguka motoni au kwenye maji. 16Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya. 17Yesu akajibu akisema, “Enyi Kizazi kisichoamini na kilichoharibika, nitakaa pamoja nanyi mpaka lini? Nitavumiliana nanyi hata lini? Mlete hapa kwangu.” 18Yesu alimkemea, na pepo akamtoka. Kijana aliponywa tangu saa ile. 19Kisha wanafunzi wakamjia Yesu kwa siri na kumwuliza, “Kwanini hatukuweza kumfukuza?” 20Yesu akawaambia, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Kweli nawaambieni, kama mtakuwa na imani hata ndogo kama punje ya mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu, hama kutoka hapa uende kule, nao utahama na hakutakuwa na kitu chochote cha kushindikana kwenu. 22Wakati wakiwa bado Galilaya, Yesu akawaambia Wanafunzi wake, “Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa watu. 23Na watamwua, na siku ya tatu atafufuka.” Wanafunzi walihuzunika sana.

Injili (Picha Isiyochorwa kwa Mikono)

Lk 9:51–56; 10:22–24

51Ikatokea kwamba, kulinga na siku zilivyokua zikikaribia zsiku zake za kwenda mbinguni, kwa uimara alielekeza uso wake Yerusalemu. 52Akatuma wajumbe mbele yake, nao wakaenda na kuingia katika kijiji cha Wasamaria ili wamtayarishie mahali. 53Lakini watu huko hawakumpokea, kwasababu alikua ameelekeza uso wake Yerusalemu. 54Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipo liona hili, wakasema, “Bwana unahitaji tuamuru moto ushuke chini kutoka mbinguni uwateketeze?” 55Lakini aliwageukia akawakemea. 56Kisha walikwenda kijiji kingine. 10:22“Kila kitu kimekabidhiwa kwangu na Baba yangu, na hakuna afahamuye Mwana ni nani ila Baba, na hakuna afahamuye Baba ni nani ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana hutamani kujifunua kwake.” 23Akawageukia wanafunzi, akasema faraghani, “Wamebarikiwa wayaonayo haya ambayo ninyi mnayaona. 24Ninawambia ninyi, kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuona mambo myaonayo, na hawakuyaona, na kusikia kusikia mnayoyaikia, na hawakuyasikia.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 29 Agosti

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 16 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 29 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki