Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 30 Agosti

Kalenda ya Kiorthodoksi · 17 Agosti (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 30 Agosti 2027

Jumatatu · Wiki ya 11 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1

Sikukuu na watakatifu

Baada ya Sikukuu ya Kulala kwa Mama Mtakatifu Sana wa Mungu

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

2 Kor 2:3–15

3Niliandika kama nilivyofanya ili kwamba wakati nikija kwenu nisiweze kuumizwa na wale ambao wangekuwa wamenifanya nifurahi. Ninao ujasiri kuhusu ninyi nyote kwamba furaha yangu ni furaha ile ile mliyonayo ninyi nyote. 4Kwa kuwa niliwaandikia ninyi kutokana na mateso makubwa, na dhiki ya moyo, na kwa machozi mengi. Sikutaka kuwasababishia ninyi maumivu. Badala yake, nilitaka mjue upendo wa kina nilionao kwa ajili yenu. 5Kama kuna yeyote amesababisha maumivu, hajasababisha tu kwangu, lakini kwa kiwango fulani - bila kuweka ukali zaidi - kwenu ninyi nyote. 6Hii adhabu ya mtu huyo kwa wengi inatosha. 7Kwa hiyo sasa badala ya adhabu, mnapaswa kumsamehe na kumfariji. Fanyeni hivi ili kwamba asiweze kushindwa na huzuni iliyozidi. 8Kwa hiyo ninawatia moyo kuthibitisha upendo wenu hadharani kwa ajili yake. 9Hii ndiyo sababu niliandika, ili kwamba niweze kuwajaribu na kujua kuwa kama ni watii katika kila kitu. 10Kama mkimsamehe yeyote, na mimi pia namsamehe mtu huyo. Kile nilicho kisamehe - kama nimesamehe chochote-kimesamehewa kwa faida yenu katika uwepo wa Kristo. 11Hii ni kwamba Shetani asije akatufanyia madanganyo. Kwa kuwa sisi sio wajinga kwa mipango yake. 12Mlango ulifunguliwa kwangu na Bwana nilipokuja kwenye mji wa Troa kuhubiri injili ya Kristo pale. 13Hata hivyo, sikuwa na amani ya moyo, kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito pale. Hivyo niliwaacha na nikarudi Makedonia. 14Lakini ashukuriwe Mungu, ambaye katika Kristo mara zote hutuongoza sisi katika ushindi. Kupitia sisi husambaza harufu nzuri ya maarifa yake mahala pote. 15Kwa kuwa sisi kwa Mungu, ni harufu nzuri ya Kristo, wote kati ya wale waliookolewa na kati ya wale wanaoangamia.

Injili

Mt 23:13–22

13Lakini ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnawafungia watu ufalme wa mbinguni. Nanyi hamwezi kuuingia, na hamwaruhusu wanaoingia kufanya hivyo. 15Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnavuka ngambo ya bahari na kufika kumfanya mtu mmoja aamini yale mnayoyafundisha, na anapokuwa kama ninyi, mnamfanya mara mbili mwana wa jehanamu kama ninyi wenyewe mlivyo. 16Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao,, Yeyote aapaye kwa hekalu, si kitu. Lakini anayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amefungwa na kiapo chake. 17Enyi vipofu wapumbavu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, dhahabu au hekalu ambalo limeweka wakfu dhahabu kwa Mungu? 18Na, yeyote aapaye kwa madhabahu, si kitu. Bali anayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amefungwa na kiapo chake. 19Enyi watu vipofu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, sadaka au madhabahu ambayo huweka wakfu sadaka zinazotolewa kwa Mungu? 20Kwa hiyo, yeye aapaye kwa madhabahu huapa kwa hiyo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake. 21Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo na kwa yeye akaaye ndani yake. 22Na yeye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketie juu yake.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 30 Agosti

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 17 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 30 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki