Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 27 Agosti
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 27 Agosti 2027
Ijumaa · Juma la 21 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Ijumaa ya Juma la 21 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Monika · Kumbukumbu
Kufunga na toba
Siku ya toba
Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Hatimaye, ndugu, twawatia moyo na kuwasihi kwa Yesu Kristo. Kama mlivyopokea maelekezo toka kwetu namna iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kwa njia hiyo pia muenende na kutenda zaidi. 2Kwa kuwa mwajua ni maelekezo gani tuliyowapa kupitia Bwana Yesu. 3Kwa kuwa haya ndiyo mapenzi ya Mungu: utakaso wenu - kwamba muepuke zinaa, 4Kwamba kila mmoja wenu anajua namna ya kumiliki mke wake mwenyewe katika utakatifu na heshima. 5Usiwe na mke kwa ajili ya tamaa za mwili (kama Mataifa wasiomjua Mungu). 6Asiwepo mtu yeyote atakaye vuka mipaka na kumkosea nduguye kwa ajili ya jambo hili. Kwa kuwa Bwana ndiye mwenye kulipa kisasi kwa mambo yote haya, kama tulivyo tangulia kuwaonya na kushuhudia. 7Kwa kuwa Bwana hakutuita kwa uchafu, bali kwa utakatifu. 8Kwa hiyo anayelikataa hili hawakatai watu, bali anamkataa Mungu, anayewapa Roho Mtakatifu wake.
Wimbo wa katikati
1Yahwe anatawala; nchi ishangilie; visiwa vingi na vifurahi. 2Mawingu na giza vyamzunguka. Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake. 5Milima huyeyuka kama nta mbele za Yahwe, Bwana wa dunia yote. 6Mbingu hutangaza haki yake, na mataifa yote huuona utukufu wake. 10Ninyi ambao mnampenda Yahwe, chukieni uovu! Yeye hulinda uhai wa watakatifu wake, naye huwatoa mikononi mwa waovu. 11Nuru imepandwa kwa ajili ya wenye haki na furaha kwa ajili ya wanyoofu wa moyo. 12Furahini katika Yahwe, enyi wenye haki; na mpeni shukurani mkumbukapo utakatifu wake.
Injili
1Ndipo ufalme wa mbinguni utafananishwa na wanawali kumi waliochukua taa zao na kuondoka kwenda kumpokea bwana harusi. 2Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano wengine walikuwa werevu. 3Wanawali wapumbavu walipochukua taa zao, hawakuchukua mafuta yoyote. 4Bali wanawali welevu walichukua vyombo vyenye mafuta pamoja na taa zao. 5Sasa wakati bwana harusi amechelewa kufika, wote walishikwa usingizi na wakalala. 6Lakini wakati wa usiku wa manane kulikuwa na yowe, 'Tazama, bwana harusi! Tokeni nje mkampokee.' 7Ndipo hao wanawali waliamka wote na kuwasha taa zao. 8Wale wapumbavu waliwaambia wale welevu, 'Mtupatie sehemu ya mafuta yenu kwa sababu taa zetu zinazimika.' 9Lakini wale welevu waliwajibu na kuwaambia, 'Kwa kuwa hayatatutosha sisi na ninyi, badala yake nendeni kwa wanaouza mjinunulie kiasi kwa ajili yenu.' 10Wakati wameenda huko kununua, Bwana harusi alifika, na wote waliokuwa tayari walienda naye kwenye sherehe ya harusi, na mlango ulifungwa. 11Baadaye wale wanawali wengine pia walifika na kusema, 'Bwana, bwana, tufungulie.' 12Lakini alijibu na kusema, 'Kweli nawaambia, Mimi siwajui.' 13Kwa hiyo angalieni, kwa kuwa hamjui siku au saa.
Watakatifu wa siku
- Mt. Monika
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki