Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 27 Agosti
Kalenda ya Kiorthodoksi · 14 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 27 Agosti 2027
Ijumaa · Wiki ya 10 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Kabla ya Sikukuu ya Kulala kwa Mama Mtakatifu Sana wa Mungu
Mfungo wa Kulala kwa Mama wa Mungu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
12Tunajivunia hili: ushuhuda wa dhamiri yetu. Kwa kuwa ni katika nia safi na usafi wa Mungu kwamba tulienenda wenyewe katika dunia. Tumefanya hivi hasa na ninyi, na sio katika hekima ya ulimwengu, lakini badala yake ni katika neema ya Mungu. 13Hatuwaandikii chochote ambacho hamwezi kukisoma au kuelewa. Ninaujasiri 14kwamba kwa sehemu mumekwisha kutuelewa. Na ninaujasiri kwamba katika siku ya Bwana Yesu tutakuwa sababu yenu kwa ajili ya kiburi chenu, kama vile mtakavyokuwa kwetu. 15Kwa sababu nilikuwa na ujasiri kuhusu hili, nilitaka kuja kwenu kwanza, ili kwamba muweze kupokea faida ya kutembelewa mara mbili. 16Nilikuwa napanga kuwatembelea wakati nikielekea Makedonia. Tena nilitaka kuwatembelea tena wakati nikirudi kutoka Makedonia, na kisha ninyi kunituma mimi wakati nikielekea Uyahudi. 17Nilipokuwa nafikiria namna hii, je, nilikuwa nasitasita? Je ninapanga mambo kulingana na viwango vya kibinadamu, ili kwamba niseme “Ndiyo, ndiyo” na “Hapana, hapana” kwa wakati mmoja? 18Lakini kama vile Mungu alivyo mwaminifu, hatusemi vyote “Ndiyo” na “Hapana.” 19Kwa kuwa mwana wa Mungu, Yesu Kristo, ambaye Silvano, Timotheo na mimi tulimtangaza miongoni mwenu, siyo “Ndiyo” na “Hapana.” Badala yake, yeye wakati wote ni “Ndiyo.” 20Kwa kuwa ahadi zote za Mungu ni “Ndiyo” katika yeye. Hivyo pia kupitia yeye tunasema “Amina” kwa utukufu wa Mungu.
Waraka (ya Jumamosi)
30Sasa ninawasihi, ndugu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, kwamba mshiriki pamoja nami katika maombi yenu kwa Mungu kwa ajili yangu. 31Ombeni kwamba niweze kuokolewa kutoka kwao wasio na utii katika Yudea, na kwamba huduma yangu huko Yerusalemu iweze kupokelewa na waumini. 32Ombeni kwamba ninaweza kuja kwenu kwa furaha kupitia mapenzi ya Mungu, na kwamba niweze kuwa pamoja nanyi, kupata kupumzika. 33Na Mungu wa amani awe pamoja nanyi nyote. Amina
Injili
23Siku hiyo baadhi ya Masadukayo walikuja kwa Yesu, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu. Wakamwuliza, 24wakisema, “Mwalimu, Musa alisema, Ikiwa mtu amefariki bila kuzaa watoto, ndugu yake na amrithi huyo mwanamke na ampatie mtoto kwa ajili ya ndugu yake. 25Walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa na kisha akafariki bila kuzaa watoto. Akamwachia mke nduguye. 26Kisha ndugu yake wa pili naye akafanya vivyo hivyo, kisha yule wa tatu, ikawa hivyo hadi kwa yule wa saba. 27Baada ya kufanya hivyo wote, yule mwanamke naye alifariki. 28Sasa katika ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani katika ndugu hao saba? Kwa sababu wote walimuoa.” 29Lakina Yesu aliwajibu na kuwaambia, “Mnakosea, kwa sababu hamjui Maandiko wala nguvu za Mungu. 30Kwa kuwa katika ufufuo, watu hawaoi wala kuolewa. Badala yake watu huwa kama malaika huko mbinguni. 31Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamjawahi kusoma kile ambacho Mungu alikisema kwenu, akisema, 32Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.” 33Wakati kusanyiko waliposikia hili, waliyashangaa mafundisho yake.
Injili (ya Jumamosi)
24Nao walipofika Kapenaumu, watu wakusanyao kodi ya nusu shekeli wakamwendea Petro na kusema, “Je mwalimu wenu hulipa kodi ya nusu shekeli?” 25Akasema, “Ndiyo” Lakini Petro alipoingia ndani ya nyumba, Yesu akaongea na Petro kwanza na kusema, “ Unafikiria nini Simon? Wafalme wa dunia, hupokea kodi au ushuru kutoka nani? Kwa wale wanaowatawa kutoka kwa wageni? 26Na wakati Petro aliposema, “Kutoka kwa wageni” Yesu akamwambia, hivyo watawaliwa wameondolewa katika ulipaji. 27Lakini tusije tukawafanya watoza ushuru wakatenda dhambi, nenda baharini, tupa ndoano, na umtwae yule samaki ajaye kwanza. Baada ya kuufungua mdomo wake, utakuta mle shekeli moja. Ichukue na uwape watoza ushuru kwa ajili yangu na wewe. 18:1Muda huo huo wanafunzi wakaja kwa Yesu na kumwambia, “Ni nani aliye mkubwa katika ufalme wa mbinguni?” 2Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao, 3na kusema, “Kweli nawaambieni, msipotubu na kuwa kama watoto wadogo hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu. 4Hivyo yeyote ajishushaye kama mtoto mdogo, mtu kama huyo ni mkuu katika ufalme wa mbinguni.
Watakatifu wa siku
- Nabii Mika (mmoja wa manabii 12) (karne ya 8 K.K.)
- Kuhamishwa kwa masalia ya Mtakatifu Mtawa Theodosio wa Mapango ya Kyiv (1091)
- Mfiadini wa Kikasisi Basili, Askofu wa Chernihiv, na pamoja naye Mtawa Mfiadini Mathayo na Mfiadini Aleksi (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Vladimir, padri (1920)
- Wafiadini wa Kikasisi Vladimir na Nikolao, mapadri, Mtawa Mfiadini Eleutherio, Watawa Wafiadini Eva, abesi, na Eudokia, na Mfiadini Theodoro (1927)
- Mtakatifu Mtawa Aleksanda Mwungamaji (1961)
- Mfiadini wa Kikasisi Markelo, Askofu wa Apamea (karibu 389)
- Mtakatifu Mtawa Arkadio wa Novy Torg (karne ya 11)
- Ikoni za Mama wa Mungu: ile iitwayo “Ya Mazungumzo” (1383) na ya Narva (1558)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 14 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 27 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki