Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 28 Agosti

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 28 Agosti 2027

Jumamosi · Juma la 21 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 21 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Agustino wa Hippo, askofu na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

1 The 4:9–11

9Kuhusu upendo wa ndugu, hakuna haja ya mtu yeyote kukuandikia, kwa kuwa mmefundishwa na Mungu kupendana ninyi kwa ninyi. 10Hakika, mlifanya haya yote kwa ndugu walioko Makedonia yote, lakini twawasihi, ndugu, mfanye hata na zaidi. 11Twawasihi mtamani kuishi maisha ya utulivu, kujali shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu, kama tulivyowaamuru.

Wimbo wa katikati

Zab 98:1, 7–9

1Zaburi. Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya, kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu; mkono wake wa kuume na mkono wake mtakatifu vimempa ushindi. 7Bahari na ipige kelele na vyote vilivyomo, ulimwengu na wale wakaao ndani yake! 8Mito na ipige makofi, na milima ipige kelele kwa furaha. 9Yahwe anakuja kuihukumu nchi; naye ataihukumu dunia kwa haki na mataifa kwa adili.

Injili

Mt 25:14–30

14Kwa kuwa ni sawa na mtu alipotaka kusafiri kwenda nchi nyingine. Aliwaita watumwa wake na kuwakabidhi utajiri wake. 15Mmoja wao alimpatia talanta tano, mwingine alimpa mbili, na yule mwingine alimpa talanta moja. Kila mmoja alipokea kiasi kulingana na uwezo wake, na yule mtu alisafari kwenda zake. 16Mapema yule aliyepokea talanta tano alienda kuziwekeza, na kuzalisha talanta zingine tano. 17Vilevile yule aliyepokea talanta mbili, alizalisha zingine mbili. 18Lakini mtumwa aliyepokea talanta moja, alienda zake, akachimba shimo ardhini, na kuificha fedha ya bwana wake. 19Na baada ya muda mrefu, bwana wa watumwa hao alirudi na kutengeneza mahesabu nao. 20Yule mtumwa aliyepokea talanta tano alikuja na kuleta talanta zingine tano, akasema, 'Bwana, ulinipa talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine tano.' 21Bwana wake alimwambia, 'Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vidogo. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.' 22Mtumwa aliyepokea talanta mbili alikuja na kusema, 'Bwana, ulinipa talanta mbili. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine mbili,' 23Bwana wake alimwambia, 'Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.' 24Baadaye mtumwa aliyepokea talanta moja alikuja na kusema, 'Bwana, najua kuwa wewe ni mtu mkali. Unachuma mahali ambapo hukupanda, na unavuna mahali ambapo hukusia. 25Mimi niliogopa, nikaenda zangu na kuificha talanta yako katika udongo. Tazama, unayo hapa ile iliyo yako.' 26Lakini bwana wake alijibu na kusema, 'Wewe mtumwa mwovu na mzembe, ulijua kwamba ninachuma mahali ambapo sijapanda na kuvuna mahali ambapo sikusia. 27Kwahiyo ulipaswa kuwapa fedha yangu watu wa benki, na wakati wa kurudi kwangu ningeipokea ile yangu pamoja na faida. 28Kwa hiyo mnyang'anyeni hiyo talanta na mpeni yule mtumwa aliye na talanta kumi. 29Kila mtu aliye nacho, ataongezewa zaidi-hata kwa kuzidishiwa sana. Lakini kwa yeyote asiye na kitu, hata alicho nacho atanyang'anywa. 30Mtupeni nje gizani huyo mtumwa asiyefaa, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.'

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 28 Agosti

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki