Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 23 Agosti
Kalenda ya Kiorthodoksi · 10 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 23 Agosti 2027
Jumatatu · Wiki ya 10 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kugeuka Sura kwa Bwana
Mfungo wa Kulala kwa Mama wa Mungu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
12Sasa kama Kristo alihubiriwa kama aliyefufuka kwa wafu, iweje baadhi yenu mseme hakuna ufufuo wa wafu? 13Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Kristo pia hakufufuka. 14Na kama Kristo hakufufuka, hivyo mahubiri yetu ni bure, na imani yenu ni bure. 15Na tumepatikana kuwa mashahidi wa uongo kumuhusu Mungu, kwa sababu tulimshushuhudia Mungu kinyume, kusema alimfufua Kristo, wakati hakumfufua. 16Kama ikiwa wafu hawafufuliwi, Yesu pia hakufufuliwa. 17Na kama Kristo hakufufuliwa, imani yenu ni bure na bado mko kwenye dhambi zenu. 18Hivyo hata wale waliokufa katika Kristo pia wameangamia. 19Ikiwa kwa maisha haya peke yake tunaujasiri kwa wakati ujao ndani ya Kristo, watu wote, sisi niwakuhurumiwa zaidi ya watu wote.
Injili
18Asubuhi alipokuwa anarudi mjini, alikuwa na njaa. 19Aliona mtini kandokando ya barabara. Akauendea, lakini hakupata kitu juu yake isipokuwa majani. Aliuambia, “Kusiwe na matunda kwako daima tena.” Na mara hiyo mtini ule ukanyauka. 20Wanafunzi walipoona, wakastaajabu na kusema, “Imekuwaje mtini umenyauka mara moja?” 21Yesu akajibu na kuwaambia, “Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani na bila wasiwasi, hamtafanya kile kilichofanyika kwa huo mtini tu, lakini mtauambia hata huo mlima, ' uchukuliwe na ukatupwe baharini, 'na itafanyika. 22Chochote mtakachoomba kwa sala, huku mkiamini, mtapokea.”
Watakatifu wa siku
- Wafiadini wa Roma: Laurenti, shemasi mkuu, Sisto, papa, Felisisimo na Agapito, mashemasi, na Romano (258)
- Mbarikiwa Laurenti, mjinga kwa ajili ya Kristo, wa Kaluga (1515)
- Mfiadini wa Kikasisi Vyacheslav, padri (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Athanasio, padri (1937)
- Kupatikana kwa mara ya pili na kuhamishwa kwa masalia ya Mtakatifu Mtawa Sava wa Storozhi, wa Zvenigorod (1998)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 10 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 23 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki