Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 20 Agosti
Kalenda ya Kiorthodoksi · 7 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 20 Agosti 2027
Ijumaa · Wiki ya 9 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kugeuka Sura kwa Bwana
Mfungo wa Kulala kwa Mama wa Mungu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
26Nini kifuatacho basi, kaka na dada zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana Zaburi, mafundisho, mafunuo, lugha au tafsiri. Fanyeni kila kitu ili kwamba mlijenge kanisa. 27Kama yeyote ananena kwa lugha, wawepo wawili au watatu, na kila mmoja katika zamu. Na mtu lazima atafasiri kilichosemwa. 28Lakini kama hakuna mtu wa kutafasiri, basi kila mmoja wao akae kimya ndani ya kanisa. Basi kila mmoja aongee peke yake na kwa Mungu. 29Na manabii wawili au watatu wanene, na wengine wasikilize kwa kupambanua kilichosemwa. 30Lakini aliyeketi akifunuliwa jambo katika huduma, yule ambaye alikuwa ananena na anyamaze. 31Kwa kuwa kila mmoja wenu anaweza kutoa unabii mmoja baada ya mwingine ili kwamba kila mmoja aweze kujifunza na wote waweze kutiwa moyo. 32Kwa kuwa roho za manabii ziko chini ya uangalizi wa manabii. 33Kwa kuwa Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani. Kama ilivyo katika makanisa yote ya waumini, 34imewapasa wanawake wakae kimya katika kanisa. Kwa kuwa hawaruhusiwi kuzungumza. Badala yake, wanapaswa kuwa katika unyenyekevu, kama pia sheria inavyosema. 35Kama kuna chochote wanatamani kujifunza, basi wawaulize waume zao nyumbani. Kwa kuwa ni aibu kwa mwanamke kuongea katika kanisa. 36Je neno la Mungu lilitoka kwenu? Je limewafikia ninyi tu? 37Kama mtu akijiona kuwa ni nabii au wa rohoni, inampasa ayatambue mambo ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo ya Bwana. 38Lakini asipotambua haya, mwacheni asitambuliwe. 39Hivyo basi, kaka na dada zangu, takeni sana kutoa unabii, na msimzuie mtu yeyote kunena kwa lugha. 40Lakini mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.
Injili
12Kisha Yesu akaingia katika hekalu la Mungu. akawafukuza nje wote waliokuwa wakinunua na kuuza hekaluni. Pia alipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wauza njiwa. 13Akawaambia, “Imeandikwa, 'Nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi, 'lakini ninyi mmeifanya pango la wanyang'anyi.” 14kisha vipofu na vilema wakamjia hekaluni, naye akawaponya. 17Kisha Yesu akawaacha na kwenda nje ya mji katika Bethania na kulala huko. 18Asubuhi alipokuwa anarudi mjini, alikuwa na njaa. 19Aliona mtini kandokando ya barabara. Akauendea, lakini hakupata kitu juu yake isipokuwa majani. Aliuambia, “Kusiwe na matunda kwako daima tena.” Na mara hiyo mtini ule ukanyauka. 20Wanafunzi walipoona, wakastaajabu na kusema, “Imekuwaje mtini umenyauka mara moja?”
Watakatifu wa siku
- Mtawa Mfiadini Dometio Mwajemi na wanafunzi wake wawili (363)
- Kupatikana kwa masalia ya Askofu Mtakatifu Mitrofani, Askofu wa Voronezh (1832)
- Mtakatifu Mtawa Antoni wa Optina (1865)
- Wafiadini wa Kikasisi Aleksanda, Petro, Mikaeli, Yohana, Demetrio na Aleksi, mapadri, Elisha, shemasi, na Mtawa Mfiadini Athanasio (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Basili, padri (1938)
- Wafiadini Marino na Asterio (260)
- Mtakatifu Mtawa Oro wa Thebaida (karibu 390)
- Mtakatifu Mtawa Pimeni, mwenye magonjwa mengi, wa Mapango ya Kyiv (1110)
- Mtakatifu Mtawa Merkurio wa Mapango ya Kyiv, Askofu wa Smolensk (1239)
- Mtakatifu Mtawa Pimeni, mfungaji wa Mapango ya Kyiv (karne ya 13-14)
- Mtawa Mfiadini Potamia, mtenda miujiza
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 7 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 20 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki