Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 8 Agosti
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 8 Agosti 2027
Jumapili · Juma la 19 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 19 ya Mwaka
Dominika · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
4Lakini yeye mwenyewe akaenda mwendo wa siku moja huko jangwani, akaja akakaa chini ya mti wa mretemu. Akajiombea mwenyewe kufa, akasema, “Sasa yatosha, BWANA, ichukue roho yangu, kwa kuwa mimi si mzuri kuliko mababu zangu waliokufa.” 5Kwa hiyo akalala chini ya mretemu. Ghafula malaika akamgusa na akamwambia, “Inuka ule.” 6Eliya akatazama, karibu na kichwa chake kulikuwa na mkate uliokuwa umeokwa kwa mkaa na gudulia la maji. Kwa hiyo akala na kunywa na kulala tena. 7Malaika wa BWANA akaja tena mara ya pili akamgusa na kumwambia, “Inuka ule, kwa sababu safari bado ndefu kwako.” 8Kwa hiyo akainuka na kula na kunywa, naye akasafiri kwa nguvu ya chakula hicho kwa siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi; wakati alipojifanya kuwa mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimtoa yeye nje. Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu. 2Nitamsifu Yahwe! walio onewa wasikie na kufurahi. 3Msifuni Yahwe pamoja nami, kwa pamoja tuliinue jina lake. 4Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote. 5Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu. 6Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote. 7Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa. 8Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.
Somo la pili
30Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu. Ni kwa Yeye kwamba mmewekewa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi. 31Lazima muweke mbali uchungu wote, ghadhabu, hasira, ugomvi, na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wema ninyi kwa ninyi. 32Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. 5:1Kwa hiyo muwe watu wa kumfuata Mungu, kama watoto wake wapendwao. 2Mtembee katika pendo, vilevile kama Kristo alivyotupenda sisi, alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu. Yeye alikuwa sadaka na dhabihu, kuwa harufu nzuri ya kumfurahisha Mungu.
Injili
41Kisha wayahudi wakamnung'unikia kumhusu yeye kwa sababu alisema, “Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 42Wakasema, “Huyu siyo Yesu mwana wa Yusuph, ambaye baba yake na mama yake tunamfahamu? Imekuwaje sasa anasema, 'Nimeshuka kutoka mbinguni'?” 43Yesu akajibu, akawambia, “Msinung'unikiane miongoni mwenu wenyewe. 44Hakuna mtu ajaye kwangu asipovutwa na Baba yangu aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho. 45Kwa kuwa imeandikwa katika manabii, 'Watafundishwa na Mungu.' Kila aliyesikia na amejifunza kutoka kwa Baba, huja kwangu. 46Sio kwamba kuna mtu aliyemwona Baba, isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu- amemwona Baba. 47Amini, amini yeye aaminiye anao uzima wa milele. 48Mimi ni mkate wa uzima. 49mababa zenu walikula manna jangwani, na wakafa. 50Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, ili kwamba mtu aule sehemu yake ili asife. 51Mimi ni mkate uishio ambao umeshuka kutoka mbinguni. Kama mtu yeyote akila sehemu ya mkate huu, ataishi milele. Mkate nitakao utoa ni mwili wangu kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Dominiko, padre
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki