Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 7 Agosti

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 7 Agosti 2027

Jumamosi · Juma la 18 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 18 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Kayetani, padre · Kumbukumbu ya hiari

Mt. Sisto II, papa, na wenzake, mashahidi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Kum 6:4–13

4Sikiliza, Israel: Yahwe Mungu wetu ni mmoja. 5Mtampenda Yahwe Mungu wenu kwa moyo wenu wote, kwa roho zenu zote, na kwa akili zenu zote. 6Maneno ninayowaamuru ninyi leo yatakuwa katika moyo wenu; 7na mtayafundisha kwa bidii kwa watoto wenu, mtayazungumza wakati mkaapo katika nyumba zenu, wakati mlalapo, na wakati mwinukapo. 8Utazifunga kama ishara juu ya mkono wako, nayo yatakuwa utepe kati ya macho yako. 9Utaziandika kwenye miimo ya mlango ya nyumba yako na kwenye malango. 10Wakati Yahwe Mungu wako akuleta kwenye nchi ambayo aliaapa kwa baba zako, Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, kwamba angekupa, pamoja na miji mikubwa na mizuri ambayo hamkuijenga, 11na nyumba zilizojaa kila aina ya vitu vizuri ambavyo hamkuzifanya, visima ambavyo hamkuvichimba, mashamba na miti ya mizeituni ambayo hamkuipanda, mtakula na kutosheka- 12basi iweni makini ili kwamba msije kumsahau Yahwe, aliyewaleta toka nchi ya Misri, toka nyumba ya utumwa. 13Mtamheshimu Yahwe Mungu wenu, yeye mtamwabudu, na mtaapa kwa jina lake.

Wimbo wa katikati

Zab 18:1–3, 46, 50

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi, mtumishi wa Yahwe, alipomwimbia Yahwe maneno ya wimbo huu katika ile siku ambayo Yahwe alimuokoa kutoka katika mkono wa adui zake wote na kutoka katika mkono wa Sauli. Yeye aliimba: Nakupenda, Yahwe, nguvu yangu. 2Yahwe ni mwamba wangu, ngome yangu, yeye ambaye aniwekae kweye usalama; yeye ni Mungu wangu, mwamba wangu; ninapata kimbilio kwake. Yeye ni ngao yangu, pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu. 3Nitamuita Yahwe kwa sababu anastahili kusifiwa, na nitaokolewa kutoka kwa adui zangu. 46Yahwe anaishi; mwamba wangu usifiwe. Ainuliwe Mungu wa wokovu wangu. 50Mungu hutoa ushindi mkuu kwa mfalme wake, na yeye huonyesha uaminifu wa agano lake kwa mpakwa mafuta wake, kwa Daudi na ukoo wake milele.

Injili

Mt 17:14–20

14Walipofika katika umati wa watu, mtu mmoja alimwendea, akapiga magoti mbele zake, na kumwambia, 15“Bwana, umhurumie mwanangu, maana amekuwa na kifafa na kuteseka sana. Kwa kuwa mara nyingi huanguka motoni au kwenye maji. 16Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya. 17Yesu akajibu akisema, “Enyi Kizazi kisichoamini na kilichoharibika, nitakaa pamoja nanyi mpaka lini? Nitavumiliana nanyi hata lini? Mlete hapa kwangu.” 18Yesu alimkemea, na pepo akamtoka. Kijana aliponywa tangu saa ile. 19Kisha wanafunzi wakamjia Yesu kwa siri na kumwuliza, “Kwanini hatukuweza kumfukuza?” 20Yesu akawaambia, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Kweli nawaambieni, kama mtakuwa na imani hata ndogo kama punje ya mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu, hama kutoka hapa uende kule, nao utahama na hakutakuwa na kitu chochote cha kushindikana kwenu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 7 Agosti

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki