Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 8 Agosti
Kalenda ya Kiorthodoksi · 26 Julai (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 8 Agosti 2027
Jumapili · Sauti ya 6
Sikukuu na watakatifu
Jumapili ya 7 baada ya Pentekoste
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Injili ya 7 ya Sala ya Alfajiri
1Mapema siku ya kwanza ya juma, kungali bado giza, Mariamu Magdalena alikuja kaburini; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. 2Kwa hiyo akakimbia mbio kwenda kwa Simon Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, kisha akawaambia, “wamemchukua Bwana kaburini, nasi hatujui kule walikomlaza.” 3Kisha Petro na yule mwanafunzi mwingine wakatoka, kuelekea kaburini. 4Wote walipiga mbio kwa pamoja; yule mwanafunzi mwingine alikimbia kwa kasi zaidi ya Petro nakufika kaburini wa kwanza. 5Akasimama na kisha kuangalia kaburini; akaiona ile sanda ya kitani imelala, lakini hakuingia ndani. 6Kisha Simon Petro naye akafika akaingia ndani ya Kaburi. Akaiona ile sanda ya kitani imelala pale 7na ile leso iliyokuwa kichwani pake haikuwa imelala pamoja na zile sanda za kitani bali ilikuwa imelala pembeni peke yake. 8Ndipo yule mwanafunzi mwingine naye alipoingia ndani ya kaburi; akaona na kuamini. 9Kwa kuwa hadi wakati huo walikuwa bado hawajayajua maandiko kwamba ilimlazimu Yesu afufuke tena katika wafu. 10Kisha wanafunzi wakaenda tena nyumbani kwao.
Waraka
1Sasa sisi tulio na nguvu tunapaswa kuuchukua udhaifu wa walio dhaifu, na hatupaswi kujipendeza wenyewe. 2Kila mmoja wetu ampendeze jirani yake kwani ni jambo jema, kwa lengo la kumjenga. 3Kwani hata Kristo hakujipendeza mwenyewe. Badala yake, ilikuwa kama ilivyoandikwa, “Matusi ya wale waliokutukana yamenipata mimi.” 4Kwa chochote kilichotangulia kuandikwa, kiliandikwa kwa kutuelekeza, kwa kusudi kwamba kupitia uvumilivu na kupitia kutiwa moyo na maandiko tungekuwa na ujasiri. 5Sasa Mungu wa uvumilivu na wa kutia moyo awape kuwa na nia sawa kwa kila mmoja kulingana na Yesu Kristo. 6Aweze kufanya hivi kwa nia moja muweze kumsifu kwa kinywa kimoja Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. 7Kwa hiyo mpokeeni kila mmoja, kama vile Kristo alivyowapokea, kwa utukufu wa Mungu.
Injili
27Ndipo Yesu alipokuwa akipita kutoka pale, wanaume wawili vipofu wakamfuata. Waliendelea kupaza sauti wakisema, “Tunaomba uturehemu, Mwana wa Daudi.” 28Pindi Yesu apokuwa amefika kwenye nyumba, wale vipofu wakaja kwake. Yesu akawaambia, “Mnaamini kwamba ninaweza kutenda?” Nao wakamwambia “Ndiyo, Bwana” 29Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema “Na ifanyike hivyo kwenu kama imani yenu ilivyo” 30Na macho yao yakafumbuka. Ndipo Yesu akasisitiza akawaamuru na kusema “Angalieni mtu yeyote asifahamu kuhusu jambo hili.” 31Lakini watu hawa wawili wakaondoka na kutangaza habari hizi sehemu zote za mji. 32Ndipo wale wanaume wawili walipokuwa wakienda zao, Tazama, mtu mmoja bubu aliyepagawa na pepo akaletwa kwa Yesu. 33Na pepo walipomtoka, yule mtu bubu akaanza kuongea. Umati ukashangazwa na kusema “Hii haijawahi kutokea katika Israel. 34Lakini mafarisayo walikuwa wakisema “ Kwa wakuu wa pepo, anawafukuza mapepo” 35Yesu akaenda kwenye miji yote na vijiji. Naye akaendelea kufundisha katika masinagogi, akihubiri injili ya ufalme, na kuponya magonjwa ya kila aina na udhaifu wa aina zote.
Watakatifu wa siku
- Wafiadini wa Kikasisi Hermolao, Hermipo na Hermokrate, mapadri wa Nikomedia (karibu 305)
- Mfiadini wa Kikasisi Sergio, padri (1937)
- Mtawa Mfiadini Paraskeva (138-161)
- Mtakatifu Mtawa Musa Mhungaria, wa Mapango ya Kyiv (karibu 1043)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 26 Julai katika kalenda ya kanisa ni 8 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki