Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 22 Julai
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 22 Julai 2027
Alhamisi · Juma la 16 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Mt. Maria Magdalena
Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
au: 2 Kor 5:14–17
1Usiku katika kitanda changu nilikuwa na shauku ya yeye ni mpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata. 2Nilisema binafsi, “Nitainuka na kwenda kupitia mji, kupitia mitaa na sokoni; nitamtafuta.” Nilimtafuta, lakini sikumpata. 3Walinzi walinipata walipo kuwa doria katika mji. Nikawauliza, “Mmemuona mpenzi wangu?” 4Ni baada ya mda mfupi kupita nilipo wapita nikampata ninaye mpenda. Nilimshika na sikumuacha hadi nilipo mleta nyumbani mwa mama yangu, katika chumba cha yeye aliyenichukua mimba. Mwanamke akiongea na wanawake wengine.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi, wakati yeye alipokuwa katika jangwa la Yuda. Mungu, wewe ni Mungu wangu! Ninakutafuta wewe kwa bidii, moyo wangu unakiu yako, mwili wangu unakutamani sana wewe, katika ukame na nchi iliyochoka mahali ambapo hakuna maji. 2Hivyo nimekutafuta wewe katika watu watakatifu kuona nguvu zako na utukufu wako. 3Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakusifu wewe. 4Hivyo nitakutukuza wewe niwapo hai; kwa jina lako nitainua mikono yangu juu. 5Itakuwa kana kwamba nilikula mlo wa mafuta na wenye kunona, kwa midomo ya furaha kinywa changu kitakusifu wewe, 7Kwa maana umekuwa msaada wangu, na katika uvuli wa mbawa zako ninafurahia. 8Ninashikamana nawe; mkono wako wa kuume unanisaidia.
Injili
1Mapema siku ya kwanza ya juma, kungali bado giza, Mariamu Magdalena alikuja kaburini; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. 11Hata hivyo, Mariamu alikuwa amesimama kaburini akilia, alivyokuwa akiendelea kulia alisimama kisha akatazama kaburini. 12Akaona malaika wawili wenye sura nyeupe wamekaa mmoja kichwani na mwingine miguuni mahali ambapo Yesu alikuwa amelala. 13Nao wakamwambia, “Mwanamke, kwa nini unalia?” Naye akawaambia, “Ni kwa sababu wamemchukua Bwana wangu, nami sijui walikomweka.” 14Alipokwisha sema hayo, aligeuka na kumwona Yesu akiwa amesimama. Lakini hakutambua kama huyo alikuwa Yesu. 15Naye Yesu akamwambia, “Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?” Naye huku akidhani kuwa ni mtunza bustani akamwambia, “Bwana, kama ni wewe uliyemchukua, niambie ulikomweka, nami nitamchukua.” 16Yesu akamwambia, “Mariamu.” Naye akageuka mwenyewe na kumwambia kwa Kiaramu, “Raboni,” yaani hii ni kusema, “Mwalimu.” 17Yesu akamwambia, “Usiniguse, kwani bado sijapaa kwenda kwa baba; bali uende kwa ndugu zangu ukawaambie kuwa nitapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye pia ni Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.” 18Mariamu Magdalena akaja kuwaambia wanafunzi, “Nimemwona Bwana,” na kwamba amemwambia mambo haya.
Watakatifu wa siku
- Mt. Maria Magdalena
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki