Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 21 Julai
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 21 Julai 2027
Jumatano · Juma la 16 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatano ya Juma la 16 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Laurenti wa Brindisi, padre na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Watu wakaendelea na safari kutoka Elimu, na jamii yote ya Waisraeli ikaja nyikani mwa Sinu, iliyopo katikati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili walipo toka Misri. 2Jamii yote ya Waisraeli wali walalamikia Musa na Aruni nyikani. 3Waisraeli waliwaambia, “Kama tu tungekufa kwa mkono wa Yahweh nchi ya Misri tulipo kuwa tumeketi kwenye vyombo vya nyama na tulikuwa tunakula mkate kwa tele. Maana umetuleta nyikani uuwe jamii zetu zote kwa njaa.” 4Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Nitakunyeshea mvua ya mkate. Watu wataenda na kukusanya kiasi cha siku kila siku ili niwajaribu kama wataendelea kushika sheria yangu au hapana. 5Itakuja kuwa siku ya sita, kwamba watakusanya mara mbili zaidi ya wanavyo kusanyaga, na watapika wanacholeta.” 9Musa akamwambia Aruni, “Sema kwa jamii yote ya watu wa Israeli, 'Njoo karibu ya Yahweh, kwa kuwa amesikia malalamishi yenu.'” 10Ikawa, Aruni alipo sema na jamii yote ya watu wa Israeli, wakaangalia kuelekea nyikani, na, tazama, utukufu wa Yahweh ukatokea kwenye wingu. 11Kisha Yahweh akasema na Musa na kumwambia, 12“Nimesikia malalamishi ya watu wa Israeli. Sema nao na useme, 'Jioni utakula nyama, na asubui utashiba mkate. Kisha utajua mimi ni Yahweh Mungu wako.'” 13Ikaja kuwa kwamba jioni kware wakaja juu na kufunika kambi. Asubui umande ulitanda kambini. 14Umande ulipo kwisha, pale juu ya ardhi ya nyikani kulikuwa na kama barafu iliyo ganda kwenye ardhi. 15Watu wa Israeli walipo ona, walisema mmoja kwa mwenzake, “Hii ni nini?” Hawakujua ilikuwa ni nini. Musa akawaambia, “Ni mkate Yahweh aliyo wapa mle.
Wimbo wa katikati
18Walimjaribu Mungu mioyoni mwao kwa kuomba chakula cha kuwatosheleza hamu zao. 19Waliongea dhidi ya Mungu; walisema, “Kweli Mungu anaweza kuweka meza ya chakula kwa ajili yetu jangwani? 23Lakini yeye bado aliziamuru mbingu juu na kufungua milango ya mbingu. 24Aliwanyeshea mana ili wale, na aliwapa nafaka kutoka mbinguni. 25Watu walikula mikate ya malaika. Aliwatumia chakula kingi. 26Alisababisha upepo wa mashariki kupiga mawinguni, na kwa uweza wake aliuongoza upepo wa kusini. 27Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, na ndege kama wingi wa mchanga wa baharini. 28Walianguka katikati ya kambi yao, na maeneo yote karibu na hema zao.
Injili
1Katika siku hiyo Yesu aliondoka nyumbani na kukaa kando ya bahari. 2Umati mkubwa ulikusanyika kwa kumzunguka, aliingia ndani ya mtumbwi na kukaa ndani yake. Umati wote walisimama kando ya bahari. 3Kisha Yesu alisema maneno mengi kwa mifano, Alisema, “Tazama, mpanzi alienda kupanda. 4Alipokuwa akipanda baadhi ya mbegu zilianguka kando ya njia na ndege walikuja wakazidonoa. 5Mbegu zingine zilianguka juu ya mwamba, ambapo hazikupata udongo wa kutosha. Ghafla zilichipuka kwa sababu udongo haukuwa na kina. 6Lakini jua lilipo chomoza zilichomwa kwa sababu hazikuwa na mizizi, na zilikauka. 7Mbengu zingine zilianguka kati ya miti yenye miiba. Miti yenye miiba ilirefuka juu ikaisonga. 8Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na kuzaa mbegu, zingine mara mia moja zaidi, zingine sitini na zingine thelathini 9Aliye na masikio na asikie.
Watakatifu wa siku
- Mt. Laurenti wa Brindisi, padre na mwalimu wa Kanisa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki