Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 12 Julai
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 12 Julai 2027
Jumatatu · Juma la 15 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 15 la Mwaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
8Wakati huu sasa mfalme mpya asiyemjua Yusufu aliinuka katika Misri. 9Akawaambia watu wake, “Tazama, hawa Waisraeli ni wengi na wenye nguvu kuliko sisi. 10Njooni na tukae nao kwa akili, ama sivyo wataendelea kuongezeka na kama vita ikiibuka, wataungana na adui zetu, watapigana nasi, na kisha wataondoka.” 11Hivyo wakawekea walinzi ambao waliwatesa kwa kuwatumikisha kazi ngumu. Waisraeli walijenga maghala ya miji kwa ajili ya Farao: Pishoni na Ramsei. 12Lakini kadiri Wamisri walivyowatesa, ndivyo Waisraeli waliendelea kuongezeka na kusambaa. Hivyo Wamisri wakaanza kuwaogopa Waisraeli. 13Wamisri waliwafanya Waisraeli wafanye kazi kwa nguvu nyingi. 14Waliyafanya maisha yao kuwa machungu kwa kuwafanyisha kazi ngumu kwa vinu na matofali na kwa kila aina ya kazi za shambani. Kazi zao zote zilikuwa ngumu. 22Farao akawaagiza watu wote, “Lazima mmutupe kila mtoto wa kiume anayezaliwa katika mto, lakini kila mtoto wa kike wamwache aishi.”
Wimbo wa katikati
1Wimbo wa kwenda kuabudu; wa Daudi. “Kama Yahwe asingekuwa upande wetu,” Israeli na aseme sasa, 2“Kama asingekuwa Yahwe ambaye alikuwa upande wetu wakati watu walipoinuka dhidi yetu, 3basi wangekuwa wametumeza tungali hai hasira yao lipozidi dhidi yetu. 4Maji yangetugharikisha; mto ungetuzidia. 5Kisha maji yafurikayo yangetuzamisha.” 6Atukuzwe Yahwe, ambaye hajaruhusu tuwe mawindo kwa meno yao. 7Tumetoroka kama ndege mtegoni mwa wawindaji; mtego umevunjika, nasi tumetoroka. 8Msaada wetu uko katika Yahwe, aliyeziumba mbingu na nchi.
Injili
34Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani, lakini upanga. 35Kwa kuwa nilikuja kumweka mtu apingane na baba yake, na binti dhidi ya mama yake, na mkwe dhidi ya mama mkwe wake. 36Adui wa mtu watakuwa wale wa nyumbani mwake. 37Yeye ambaye anampenda baba au mama zaidi kuliko mimi huyo hanistahili. Na yeye anayempenda kijana au binti zaidi kuliko mimi huyo hanistahili. 38Yeye ambaye hatabeba msalaba na kunifuata mimi hanistahili. 39Yeye atakayetafuta maisha atayapoteza. Lakini yeye atakayepoteza maisha kwa ajili yangu atayapata. 40Yeye atakayewakaribisha amenikaribisha mimi, na yeye atakayenikaribisha mimi amemkaribisha yeye aliyenituma mimi. 41Na yeye atakayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii atapokea thawabu ya nabii. Na yeye atakayemkaribisha mwenye haki kwa sababu ni mtu wa haki atapokea thawabu ya mtu wa haki. 42Yeyote atakayempatia mmoja wa wadogo hawa, hata kikombe cha maji ya kunywa ya baridi, kwa sababu yeye ni mwanafunzi, kweli ninawaambia, yeye hawezi kukosa kwa njia yeyote thawabu yake.” 11:1Ikawa baada ya Yesu kumaliza kuwaelekeza wanafunzi wake kumi na wawili aliondoka plae kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao,
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki