Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 10 Julai

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 10 Julai 2027

Jumamosi · Juma la 14 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 14 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Kumbukumbu ya Bikira Maria siku ya Jumamosi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mwa 49:29–32; 50:15–26

29Kisha akawaelekeza na kuwaambia, “Ninakaribia kwenda kwa watu wangu. Mnizike pamoja na babu zangu katika pango lililoko katika shamba la Efroni Mhiti, 30katika pango lililo katika shamba la Makpela, karibu na Mamre katika nchi ya Kanaani, shamba Ibrahimu alilolinunua kwa Efron Mhiti kwa ajili ya eneo la kuzikia. 31Pale walimzika Ibrahimu na Sara mkewe; pale wakamzika Isaka na Rebeka mkewe; na pale nikamzika Lea. 32Shamba na pango lililomo lilinunuliwa kutoka kwa watu wa Hethi.” 50:15Nduguze Yusufu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje ikiwa Yusufu atatukasirikia na akataka kutulipa kikamilifu kwa ajili ya uovu tuliomtenda?” 16Hivyo wakamwagiza Yusufu, kusema, “Baba yako alitoa maelekezo kabla hajafa, kusema, 17'Mwambieni hivi Yusufu, “Tafadhari samehe makosa ya ndugu zako na dhambi yao uovu waliokutenda.” Basi wasamehe watumishi wa Mungu wa baba yako.” Yusufu akalia walipomwambia. 18Ndugu zake pia wakaenda na kuinamisha nyuso zao mbele zake. Wakasema, “Tazama, sisi ni watumishi wako.” 19Lakini Yusufu akawajibu, “Msiogope, Je mimi ni badala ya Mungu? 20Lakini kwenu, mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, kuhifadhi maisha ya watu wengi, kama mwonavyo leo. 21Hivyo basi msiogope. Nitawahudumia ninyi na watoto wenu wadogo.” Kwa njia hii aliwatia moyo na kuongea na mioyo yao kwa upole. 22Yusufu akakaa Misri, pamoja na familia ya baba yake. Akaishi miaka mia moja na kumi. 23Yusufu akawaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu. Pia aliwaona wana wa Makiri mwana wa Manase, waliowekwa katika magoti ya Yusufu. 24Yusufu akawambia ndugu zake, “Ninakaribia kufa; lakini kwa hakika Mungu atawajilia na kuwaongoza kutoka katika nchi hii na kuwapeleka katika nch aliyoapa kumpa Ibrahimu, kwa Isaka na kwa Yakobo.” 25Kisha Yusufu akawaapisha watu wa Israeli kwa kiapo. Akasema, “Bila shaka Mungu atawajilia. Wakati huo mtachukuwa mifupa yangu kutoka hapa.” 26Hivyo Yusufu akafa, mwenye miaka 110. Wakampaka dawa na akawekwa katika jeneza huko Misri.

Wimbo wa katikati

Zab 105:1–4, 6–7

1Mshukuruni Yahwe, liitieni jina lake; myafanye matendo yake yajulikane kati ya mataifa. 2Mwimbieni yeye, mwimbieni sifa yeye; semeni matendo yake yote ya ajau. 3Mjivune katika utakatifu wa jina lake; moyo wao wamtafutao Yahwe ufurahi. 4Mtafuteni Yahwe na nguvu zake; utafuteni uwepo wake siku zote. 6miujiza yake na amri zitokazo kinywani mwake, enyi kizazi cha Ibrahimu mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wachaguliwa wake. 7Yeye ni Yahwe, Mungu wetu. Amri zake ziko juu ya nchi yote.

Injili

Mt 10:24–33

24Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumwa aliye juu ya Bwana wake. 25Inatosha kwa mwanafunzi kwamba awe kama mwalimu wake, na mtumishi kama Bwana wake. Ikiwa wamemwita Bwana wa nyumba Belzabuli, ni kwa kiasi gani zaidi watawakashifu wa nyumba yake! 26Hivyo basi msiwahofu wao, kwa kuwa hakuna jambo ambalo halitafunuliwa, na hakuna lililofichika ambalo halitajulikana. 27Kile ninachowaambia gizani, mkiseme nuruni, na mnachokisikia kwa ulaini masikioni mwenu, mkitangaze mkiwa juu ya nyumba. 28Msiwaogope wale ambao wanaua mwili lakini hawana uwezo wa kuua roho. Badala yake, mwogopeni yule ambaye awezaye kuangamiza mwili na roho kule kuzimu. 29Je kasuku wawili hawauzwi kwa senti ndogo? Hata hivyo hakuna anayeweza kuanguka chini bila Baba yenu kufahamu. 30Lakini hata idadi ya nywele zenu zimehesabiwa. 31Msiwe na hofu, kwa kuwa mnathamani zaidi kuliko kasuku wengi. 32Hivyo basi kila mmoja atakaye nikiri mbele za watu, nami pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 33Lakini yeye atakaye nikana mbele za watu, nami pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.

Watakatifu wa 10 Julai

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki