Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 29 Juni
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 29 Juni 2027
Jumanne · Juma la 13 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Watakatifu Petro na Paulo, mitume
Sherehe · Rangi ya liturujia: nyekundu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Wakati huo mfalme Herode akanyosha mkono wake kwa baadhi ya wale wanaotoka kwenye kusanyiko ili kuwatesa. 2Akamwuua Yakobo nduguye Yohana kwa upanga. 3Baada ya kuona kuwa inawapendeza Wayahudi, akamkamata na Petro tena. Hii ilikuwa wakati wa mikate isiyochachwa. 4Alipomkamata, akamweka gerezani na akaweka vikosi vinne vya askari ili kumlinda, alikuwa akitarajia kumpeleka kwa watu baada ya Pasaka. 5Petro akawekwa gerezani, lakini maombi yakafanywa kwa bidii na kusanyiko kwa ajili yake kwa Mungu. 6Siku kabla Herode hajaenda kumtoa, Usiku huo Petro alikuwa amelala katikati ya maaskari wawili, akiwa amefungwa na minyororo miwili, na walinzi mbele ya mlango walikuwa wakilinda gereza. 7Tazama, malaika wa Bwana ghafla akamtokea na nuru ikang'aa ndani. Akampiga Petro ubavuni na kumwamsha akisema, “Amka haraka.”ndipo minyororo aliyokuwa amefungwa ikafunguka kutoka mikononi mwake. 8Malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na vaa viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Malaika akamwambia, “Vaa vazi lako na unifuate.” 9Hivyo Petro akamfuata Malaika na akatoka nje. Hakuamini kilichofanywa na malaika kama ni cha kweli. Alidhani anaona maono. 10Baada ya kupita lindo la kwanza na la pili, wakafika kwenye geti la chuma la kuingilia kwenda mjini, likafunguka lenyewe kwa ajili yao. Wakatoka nje wakashuka kwenye mtaa, mara Malaika akamwacha. 11Petro alipojitambua, akasema, “Sasa nimeamini kuwa Bwana alimtuma Malaika wake ili kunitoa katika mikono ya Herode, na kwa matarajio ya watu wote wa uyahudi.”
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi; wakati alipojifanya kuwa mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimtoa yeye nje. Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu. 2Nitamsifu Yahwe! walio onewa wasikie na kufurahi. 3Msifuni Yahwe pamoja nami, kwa pamoja tuliinue jina lake. 4Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote. 5Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu. 6Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote. 7Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa. 8Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.
Somo la pili
6Kwa maana mimi tayari nimekwisha kumiminwa. Muda wa kuondoka kwangu umewadia. 7Nimeshindana katika haki, Mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda. 8Taji ya haki imewekwa kwa ajili yangu, ambayo Bwana, anayehukumu kwa haki, atanipa siku ile. Na siyo kwangu tu bali pia kwa wote wanaongojea kwa shauku kuonekana kwake. 17Lakini Bwana alisimama pamoja nami, akanitia nguvu ili kwamba kupitia kwangu, neno linenwe kwa ukamilifu na mataifa wapate kusikia. Niliokolewa katika kinywa cha Simba. 18Bwana ataniepusha na matendo yote maovu na kuniokoa kwa ajili ya ufalme wake wa mbinguni. Utukufu uwe kwake milele na milele. Amen
Injili
13Wakati Yesu alipofika sehemu za Kaisaria ya Filipi, akawauliza wanafunzi wake, akisema, “Watu wanasema kuwa Mwana wa Mtu ni nani?” 14Wakasema,” Wengine husema kuwa ni Yohana Mbatizaji; wengine, Eliya; na wengine, Yeremia, au mojawapo wa manabii. 15Akawaambia, ninyi mwasema mimi ni nani? 16Kwa akijibu, Simoni Petro akasema, “Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai” 17Yesu akamjibu na kumwambia, “Umebarikiwa wewe, Simoni Bar Yona, kwa kuwa damu na nyama havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18Nami pia ninakwambia kuwa wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu. Milango ya kuzimu haitalishinda. 19Nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni. Chochote utakachokifunga duniani kitakuwa kimefungwa mbinguni, na chochote utakachokifungua duniani kitafunguliwa na mbinguni.”
Watakatifu wa siku
- Watakatifu Petro na Paulo, mitume
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki