Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 15 Juni

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 15 Juni 2027

Jumanne · Juma la 11 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumanne ya Juma la 11 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

2 Kor 8:1–9

1Tunawataka ninyi mjue, kaka na dada, kuhusu neema ya Mungu ambayo imetolewa kwa makanisa ya Makedonia. 2Wakati wa jaribu kubwa la mateso, wingi wa furaha yao na ongezeko la umaskini wao umezaa utjiri mkubwa wa ukarimu. 3Kwa maana nashuhudia kwamba walitoa kwa kadiri ya walivyoweza, na hata zaidi ya walivyoweza. 4Na kwa hiari yao wenyewe kwa kutusihi kwingi, walituomba kwa ajili ya kushiriki katika huduma hii kwa waumini. 5Hii haikutokea kama tulivyokuwa tunatarajia. Badala yake, kwanza walijitoa wao wenyewe kwa Bwana. Kisha wakajitoa wao wenyewe kwetu kwa mapenzi ya Mungu. 6Hivyo tulimsihi Tito, aliyekuwa tayari ameanzisha kazi hii, kuleta katika utimilifu tendo hili la ukarimu juu yenu. 7Lakini ninyi mna wingi katika kila kitu- katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika bidii, na katika upendo wenu kwa ajili yetu. Hivyo hakikisheni kwamba ninyi mnakuwa na wingi pia katika tendo hili la ukarimu. 8Nasema hili si kama amri. Badala yake, nasema hili ili kupima uhalisi wa upendo wenu kwa kuulinganisha na shauku ya watu wengine. 9Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Hata kama alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikuwa maskini. Ili kwamba kupitia umaskini wake mweze kuwa tajiri.

Wimbo wa katikati

Zab 146:1–2, 5–9

1Msifu Yahwe. Msifu Yahwe, ee nafsi yangu. 2Ninamsifu Mungu maisha yangu yote; nitamuimbia sifa Mungu wangu ni ngali ni hai. 5Amebarikiwa yule ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake liko katika Yahwe Mungu wake. 6Yahwe aliumba mbingu na nchi, bahari, na vyote vilivyomo; huitazama kweli milele. 7Yeye hutekeleza hukumu kwa ajili ya walioonewa na huwapa chakula wenye njaa. Yahwe huwafungua waliofungwa; 8Yahwe huyafungua macho ya kipofu; Yahwe huwainua walioinama; Yahwe huwapenda watu wenye haki. 9Yahwe huwalinda wageni katika nchi; huwainua yatima na wajane, bali huipinga njia ya wasio haki.

Injili

Mt 5:43–48

43Mmesikia imenenwa, 'Umpende jirani yako, na umchukie adui yako.' 44Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi, 45Ili kwamba muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni. Kwa kuwa anafanya jua liwaangazie wabaya na wema, na anawanyeshea mvua waovu na wema. 46Kama mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Kwani watoza ushuru hawafanyi hivyo? 47Na kama mkiwasalimia ndugu zenu tu mwapata nini zaidi ya wengine? Je!, Watu wa mataifa hawafanyi vivyo hivyo? 48Kwa hiyo yawapasa kuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Watakatifu wa 15 Juni

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki