Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 25 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 25 Mei 2027

Jumanne · Juma la 8 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumanne ya Juma la 8 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Beda Mheshimiwa, padre na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu ya hiari

Mt. Gregori VII, papa · Kumbukumbu ya hiari

Mt. Maria Magdalena de Pazzi, bikira · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 50:5–8, 14, 23

5Kwa pamoja kusanyikeni waaminifu wangu kwangu, wale waliofanya nami agano kwa sadaka.” 6Mbingu zitatangaza haki yake, kwa maana Mungu mwenyewe ndiye jaji. Serah 7Sikilizeni, watu wangu, nami nitazungumza; mimi ni Mungu, Mungu wenu. 8Sitawakaripia ninyi kwa ajili ya sadaka zenu; sadaka zenu za kuteketeza ziko nami siku zote. 14Mtoleeni Mungu sadaka za shukurani, na mlipe viapo vyenu kwa Aliye Juu. 23Yule atoaye sadaka ya shukurani hunitukuza, na yeyote apangaye njia zake katika namna iliyo sahihi nitamuonesha wokovu wa Mungu.”

Injili

Mk 10:28–31

28“Petro akaanza kuzungumza naye, “Angalia tumeacha vyote na tumekufuata.” 29Yesu akasema, “Ukweli nawaambia ninyi, hakuna aliyeacha nyumba, au kaka, au dada, au mama, au baba, au watoto, au ardhi, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, 30ambaye hatapokea mara mia zaidi ya sasa hapa duniani: nyumba, kaka, dada, mama, watoto, na ardhi, kwa mateso, na ulimwengu ujao, uzima wa milele. 31Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 25 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki