Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 28 Aprili

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 28 Aprili 2027

Jumatano · Juma la 5 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 5 la Pasaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Ludoviko Grignion de Montfort, padre · Kumbukumbu ya hiari

Mt. Petro Chanel, padre na shahidi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 15:1–6

1Watu fulani walishuka kutoka Uyahudi na kuwafundisha ndugu, wakisema, “msipotahiriwa kama desturi ya Musa, hamwezi kuokolewa.” 2Wakati Paulo na Barnaba walipokuwa na mapambano na mjadala pamoja nao, ndugu waliamua kwamba Paulo, Barnaba, na wengine kadhaa waende Yerusalem kwa mitume na wazee kwa ajili ya swali hili. 3Kwa hiyo, kwa kutumwa kwao na kanisa, walipitia Foinike na Samaria wakitangaza kugeuzwa nia kwa wamataifa. Walileta furaha kuu kwa ndugu wote, 4Walipokuja Yerusalem, walikaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, na waliwasilisha taarifa ya mambo yote ambayo Mungu amefanya pamoja nao. 5Lakini watu fulani walioamini, waliokuwa katika kundi la Mafarisayo, walisimama nakusema, “ni muhimu kuwatahiri na kuwaamuru waishike sheria ya Musa.” 6Hivyo mitume na wazee walisimama pamoja kulifikiria hili swala.

Wimbo wa katikati

Zab 122:1–2, 4–5

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi. Nilifurahi waliponiambia, “Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe.” 2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako! 4Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe. 5Huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.

Injili

Yn 15:1–8

1Mimi ni mzabibu wa huu kweli, na baba yangu ni mkulima wa mzabibu. 2Kila tawi ndani yangu ambalo halizai tunda, na husafisha kila tawi ambalo huzaa tunda huliondoa ili kwamba liweze kuzaa zaidi. 3Ninyi tayari mmekuwa safi kwa sababu ya ujumbe ambao nimekwisha waambia. 4Mkae ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama tawi lisivyoweza kuzaa peke yake lisipo kuwa katika mzabibu, kadhalika nayi, msipo kaa ndani yangu. 5Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Adumuye ndani yangu na mimi ndani yake, mtu huyu huzaa matunda mengi, kwa kuwa pasipo mimi hamuwezi kufanya jambo lolote. 6Ikiwa mtu yeyote hatasalia ndani yangu, atatupwa kama tawi na kukauka; watu hukusanya matawi na kuyatupa katika moto, na kuteketea. 7Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa. 8Katika hili baba yangu ametukuzwa, kwamba mnazaa matunda mengi na kwamba ni wanafunzi wangu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 28 Aprili

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki