Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 13 Machi
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 13 Machi 2027
Jumamosi · Juma la 4 la Kwaresima
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 4 la Kwaresima
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: zambarau
Masomo ya siku
Somo la kwanza
18Bwana alinijulisha mambo haya, kwa hiyo nakayajua. Wewe, Bwana, umenifanya nione matendo yao. 19Nilikuwa kama kondoo mpole unayeongozwa na mchinjaji. Sikujua kwamba walikuwa wameunda mipango dhidi yangu, “Hebu tuangamize mti na matunda yake! Hebu tumkatilie mbali na nchi ya walio hai ili jina lake lisikumbukwe tena. 20Lakini Bwana wa majeshi ndiye mwamuzi mwenye haki ambaye huchunguza moyo na akili. Mimi nitashuhudia kisasi chako dhidi yao, kwa kuwa nimekuletea kesi yangu kwako.
Wimbo wa katikati
1Utungo wa muziki wa daudi, ambao alimwimbia Yahwe kuhusu maneno ya Cush Mbenjamini Yahweh Mungu wangu, kwako napata kimbilio! Uninusuru na hao wote wanikimbizao, na uniokoe. 2Vinginevyo, watanipura kama simba, na kunitawanya viapande vipande na asiwepo mtu wa kuweza kunirudisha katika usalama. 8Yahweh, uwahukumu mataifa; uwaonyeshe kuwa sina hatia, Yahweh, kwa sababu mimi ni mwenye haki na sina hatia, Ewe uliye juu. 9Matendo ya waovu na yafike mwisho, bali uanzishe watu wenye haki, Mungu mwenye haki, wewe ambaye unapima mioyo na fahamu. 10Ngao yangu inatoka kwa Mungu, yule anaye okoa moyo wa mwenye haki. 11Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu anaye chukizwa na waovu kila siku.
Injili
40Baadhi ya makutano, waliposikia maneno haya, walisema, “Kweli huyu ni nabii.” 41Wengine walisema, “Huyu ni Kristo.” Lakini wengine walisema, “nini, Kristo aweza kutoka Galilaya? 42Maandiko hayajasema kuwa Kristo atatokea katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi alikuwa? 43Hivyo, pale ukainuka mgawanyiko katikati ya makutano kwa ajili yake. 44Wengine kati yao wangelimkamata, lakini hakuna aliyenyoosha mikono yake juu yake. 45Ndipo wale maofisa wakarudi kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, nao wakawaambia, “Kwa nini hamjamleta?” 46Maofisa wakajibu, “Hakuna mtu aliyewahi kuzungumza kama huyu kabla.” 47Ndipo Mafarisayo walipowajibu, “Na nyinyi pia mmepotoshwa? 48Kuna yeyote kati ya watawala anayemwamini, au yeyote wa Mafarisayo? 49Bali hawa makutano wasiojua sheria - wamelaaniwa.” 50Nikodemo akawaambia (yeye aliyemwendea Yesu zamani, akiwa mmoja wa Mafarisayo), 51“Je sheria yetu inamhukumu mtu isipokuwa amesikilizwa kwanza na kujua anachokifanya?” 52Walijibu na kumwambia, “Na wewe pia unatokea Galilaya? Tafuta na uone kwamba hakuna nabii aliyetokea Galilaya.” 53Kisha kila mtu alienda nyumbani kwake.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki