Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 14 Machi

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 14 Machi 2027

Jumapili · Juma la 5 la Kwaresima

Sikukuu na watakatifu

Dominika ya 5 ya Kwaresima

Dominika · Rangi ya liturujia: zambarau

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Yer 31:31–34

31Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—nitakapoanzisha aganao jipya pamaoja na nyumba aya Israeli na nyumba ya Yuda. 32Halitakuwa kama agano ambalo nilianzisha na baba zao nilipowatoa kwa mkono wao nje ya nchi ya Missiri. Hizo zzilikuwa siku ambapo walilivunja aaganao lanaahu, ingawa nilikuwa mme kwao—hili ni tangazo la Yahwe. 33Lakaini hili ni agano nitakaloanzisha na nyumba ya Israeli baada ya siku hizi—hili ni tangazo la Yahwe: Nitaiweka sheria yangu ndani yao na nitaiandika juu ya mioyo yao, kwa maana nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watau wangu. 34Kisha kila mtu hatamfundisha jiranai yake, wala mtu hatamfundisha ngugu yake akisema, 'Mjue Yahwe!' Kwa maana wao wote, kuanzia mdogo wao hata mkubwa, watanijua—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitawasamehe uovu wao na sitazikumbuka tena dhambi zao.”'

Wimbo wa katikati

Zab 51:1–2, 10–13

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi; wakati nabii Nathani amekuja kwake baada ya kusikia kuwa alilala na Bathsheba. Unirehemu, Mungu, kwa sababu ya uaminifu wa agano lako; kwa ajili ya wingi wa matendo yako ya rehema, uyafute makosa yangu. 2Unioshe kabisa uovu wangu na unisafishe dhambi zangu. 10Uniumbie moyo safi, Mungu, na uifanye upya roho ya haki ndani yangu. 11Usiniondoe uweponi mwako, na usimuondoe roho Mtakatifu ndani yangu. 12Unirudishie furaha ya wokovu wako, na unihifadhi mimi kwa roho ya utayari. 13Ndipo nitawafundisha wakosaji jia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.

Somo la pili

Ebr 5:7–9

7Wakati wa kipindi chake katika mwili, aliomba na kuombea, alimwomba Mungu kwa machozi, kwa yeye awezaye kumwokoa kutoka kwenye kifo. Kwa sababu ya unyenyekevu wake kwa Mungu, alisikiwa. 8Ijapokuwa alikua mwana, alijifunza kutii kwa mambo yaliyomtesa. 9Alikamilishwa na kwa njia hii alifanyika kwa kila mtu amwaminiye kuwa sababu ya wokovu wa milele,

Injili

Yn 12:20–33

20Sasa baadhi ya Wayunani walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakienda kuabudu kwenye sikukuu. 21Hawa walimwendea Filipo, ambaye alitoka Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba wakisema, “Bwana, sisi tunatamani kumwona Yesu.” 22Filipo akaenda akamwambia Andrea; Andrea na Filipo wakaenda na kumwambia Yesu. 23Yesu akawajibu akasema, “Saa imefika kwa ajili ya Mwana wa Adamu kutukuzwa. 24Amini, amini, nawaambia, chembe ya ngano isipoanguka katika nchi ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, itazaa matunda mengi. 25Yeye apendaye uhai wake ataupoteza; bali yeye auchukiaye uhai wake katika ulimemngu huu atausalimisha hata uzima wa milele. 26Mtu yeyote akinitumikia mimi, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Mtu yeyote akinitumikia, Baba atamheshimu. 27Sasa roho yangu imefadhaika: nami nisemeje? 'Baba, uniokoe katika saa hii'? Lakini ni kwa kusudi hii nimeifikia saa hii. 28Baba, ulitukuze jina lako.” Kisha sauti ikaja kutoka mbinguni na kusema, “Nimelitukuza nami nitalitukuza tena.” 29Basi mkutano uliosimama karibu naye wakasikia, wakasema ya kwamba kumekuwa ngurumo. Wengine walisema, “Malaika amesema naye.” 30Yesu akajibu na kusema, “Sauti hii haikuja kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu. 31Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo: Sasa mkuu wa ulimwngu huu atatupwa nje. 32Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.” 33Aliyanena hayo akionesha ni mauti gani atakayokufa.

Watakatifu wa 14 Machi

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki