Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 12 Machi
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 12 Machi 2027
Ijumaa · Juma la 4 la Kwaresima
Sikukuu na watakatifu
Ijumaa ya Juma la 4 la Kwaresima
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: zambarau
Kufunga na toba
Kujinyima nyama
Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.
Masomo ya siku
Somo la kwanza
Haimo katika tafsiri hii
Wimbo wa katikati
16Uso wa Yahwe uko kinyume na wale watendao uovu, kuikatilia mbali kumbukumbu yao duniani. 17Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote. 18Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni. 19Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote. 20Yeye huitunza mifupa yake yote, hakuna hata mmoja wao utavunjika. 22Yahwe huokoa maisha ya watumishi wake. Hakuna atakaye hukumiwa hata mmoja atafutaye usalama katika yeye.
Injili
1Na baada ya mambo haya Yesu alisafiri hivi katika Galilaya, kwa sababu hakupenda kwenda Uyahudi kwa sababu wayahudi walikuwa wakifanya mipango ya kumwua. 2Sasa sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu. 10Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri. 25Baadhi yao kutoka Yerusalemu wakasema, “Siye huyu wanayemtafuta kumwua? 26Na tazama, anaongea wazi wazi, na hawasemi chochote juu yake. Haiwezi ikawa kwamba viongozi wanajua kweli kuwa huyu ni Kristo, inaweza kuwa? 27Tunajua huyu mtu anatokea wapi. Kristo atakapokuja, hata hivyo, hakuna atakayejua wapi anakotoka.” 28Yesu alikuwa akipaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, “Ninyi nyote mnanijua mimi na mnajua nitokako. Sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye aliyenituma ni wa kweli, na hamumjui yeye. 29Ninamjua yeye kwa sababu nimetoka kwake na alinituma.” 30Walikuwa wanajaribu kumkamata, lakini hakuna hata mmoja aliyeinua mkono wake juu yake kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki