Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 23 Februari

Kalenda ya Kiorthodoksi · 10 Februari (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 23 Februari 2027

Jumanne · Wiki ya Mtoza Ushuru na Farisayo · Sauti ya 5

Sikukuu na watakatifu

Mfiadini wa Kikasisi Haralampo na pamoja naye Wafiadini Porfirio, Bapto, Theoktisto na wanawake watatu wafiadini (202)

Wiki isiyo na mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

2 Pet 2:9–22

9Kwa hiyo Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wake wakati wa mateso na jinsi ya kuwavumilia waovu kwa ajili ya hukumu katika siku ya mwisho. 10Kwa hakika huu ndio ukweli kwa wale wanoendelea kuishi katika tamaa za mwili huu na kuyadharau mamlaka. Watu wa jinsi hii wana ujasiri katika dhamiri zao, Hawaogopi kuwakufuru watukufu. 11Ingawa malaika wana uwezo na nguvu kuliko wanadamu, lakini hawawezi kuleta hukumu dhidi yao kwa Bwana 12Lakini hawa wanyama wasio na akili wametengenezwa kwa asili ya kukamatwa na kuangamizwa. 13Wanaumizwa kwa ujira wa maovu yao. Mchana kutwa huishi kwa anasa. Wamejaa uchafu na maovu. Hufurahia anasa za udanganyifu wanaposherehekea na wewe. 14Macho yao yamefunikwa na uzinzi; hawatosheki kutenda dhambi. Huwalaghai na kuwaangusha waumini wachanga katika dhambi. Wana mioyo iliyojaa tamaa, ni watoto waliolaaniwa. 15Wameiacha njia ya kweli. wamepotoka na wameifuata njia ya Balaam mwana wa Beori, aliyependa kupata malipo ya udhalimu. 16Lakini alikemewa kwa ajili ya ukosai wake. Punda aliyekuwa bubu akiongea katika sauti ya binadamu, alizuia wazimu wa nabii.. 17Watu hawa ni kama chemichemi zisizo na maji. Ni kama mawingu yanayotoweshwa na upepo. Wingu zito limehifadhiwa kwa ajili yao. 18Huongea kwa majivuno matupu. Huwaangusha watu kwa tamaa ya mwili. Huwalaghai watu wanaojaribu kuwakimbia wale waishio katika ukosaji. 19Huwaahidi watu uhuru wakati wao wenyewe ni watumwa wa dhambi ya ufisadi. Maana mwanadamu hufanywa kuwa mtumwa wa kile kinachomtawala. 20Yeye ajiepushaye na uchafu wa ulimwengu kwa kutumia maarifa ya Bwana na mwokozi Yesu Kristo, na kisha akarudia uchafu huo tena, hali yake huwa mbaya kuliko ile ya mwanzo. 21Ingefaa watu hao kama wasingeifahamu njia ya haki kuliko kuifahamu na kisha tena kuziacha amri takatifu walizopewa. 22Mithali hii huwa na ukweli kwao. “mbwa huyarudia matapishi yake. Na nguruwe aliyeoshwa hurudi tena kwenye matope.”

Injili

Mk 13:14–23

14Mtakapoona chukizo la uharibifu limesimama pale lisipotakiwa kusimama (asomaye na afahamu), ndipo walioko ndani ya Yuda wakimbilie milimani, 15naye aliyeko juu ya nyumba asishuke chini ya nyumba, au kuchukua chochote kilichoko nje, 16na aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake. 17Lakini ole wao wanawake wenye mimba na wanyonyeshao katika siku hizo! 18Ombeni kwamba isitokee wakati wa baridi. 19Kwani patakuwa na mateso makubwa, ambayo hayajawahi kutokea, tangu Mungu alipoumba ulimwengu, mpaka sasa, hapana, wala haitatokea tena. 20Mpaka Bwana atakapopunguza siku, hakuna mwili utakaookoka, lakini kwa ajili ya wateule, atakaowachagua, atapunguza namba za siku. 21Wakati huo kama mtu yeyote atawaambia, Tazama, Kristo yuko hapa!' au 'Tazama, yuko pale!' msiamini. 22Kwani Wakristo wa uongo na manabii wa uongo watatokea na watatoa ishara na maajabu, ili kwamba, wawadanganye, yamkini hata wateule. 23Iweni macho! Nimekwisha wambia haya yote kabla ya wakati.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 23 Februari

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 10 Februari katika kalenda ya kanisa ni 23 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki