Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 23 Februari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 23 Februari 2027
Jumanne · Juma la 2 la Kwaresima
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 2 la Kwaresima
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: zambarau
Mt. Polikarpo, askofu na shahidi · Ukumbusho
Masomo ya siku
Somo la kwanza
10Sikiliza neno la Yahwe, enyi viongozi wa Sodomu; sikilizeni sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora: 16Jiosheni, jitakaseni wenyewe; ondoeni matendo maovu mbele ya macho yangu; acheni kutenda dhambi; 17jifunze kutenda mema; tafuta ukweli; msiwanyanyase, wapeni haki yatima, walindeni wajane.'' 18Njooni sasa, njooni tusemezane, asema Yahwe, japokuwa dhambi zenu ni nyekundu kama bendera zitakuwa nyeupe kama theluji; japokuwa ni myekundu kama damu zitakuwa kama sufi. 19Kama utakubali na kutii, utakula mema ya nchi, 20lakini ukikataa na kugeuka, upanga utakuangamiza, maama Yahwe amesema.
Wimbo wa katikati
8Sitawakaripia ninyi kwa ajili ya sadaka zenu; sadaka zenu za kuteketeza ziko nami siku zote. 9Sitachukua ng'ombe katika nyumba yenu, wala beberu katika mazizi yenu. 16Lakini kwa waovu Mungu anasema, “Inawahusu nini kuitangaza hali yangu, kwamba ninyi mmeliweka agano langu mdomoni mwenu, 17wakati ninyi mnayachukia maelekezo na mnayatupa maneno yangu? 21Mmefanya mambo haya, lakini nimekaa kimya, hivyo mlidhani kuwa ni mtu flani nilliye kama ninyi mlivyo. Lakini nitawakaripia ninyi na kuwafunua, mbele ya macho yenu, mambo yote miliyofanya. 23Yule atoaye sadaka ya shukurani hunitukuza, na yeyote apangaye njia zake katika namna iliyo sahihi nitamuonesha wokovu wa Mungu.”
Injili
1Baadaye aliongea na umati wa watu na wanafunzi wake. Akasema, 2“Waandishi na Mafarisayo wanakalia kiti cha Musa. 3Kwa hiyo chochote wanacho waamuru kufanya, fanyeni huku mkiwachunguza. Lakini msije mkaiga matendo yao, kwa sababu wao hutamka mambo wasiyoyafanya. 4Kweli, wao hufunga mizigo mizito ambayo ni vigumu kuibeba, na kisha huwabebesha watu mabegani mwao. Lakini wao wenyewe hawasogezi hata kidole kuibeba. 5Matendo yao yote, huyafanya ili watazamwe na watu. Kwa sababu wao hupanua masanduku yao na huongeza ukubwa wa mapindo ya mavazi yao. 6Wao hupendelea kukaa maeneo ya kifahari katika sherehe na katika viti vya heshima ndani ya masinagogi, 7na kusalimiwa kwa heshima maeneo ya sokoni, na kuitwa “Walimu” na watu. 8Lakini ninyi hampaswi kuitwa “Walimu,” Kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja, na ninyi wote ni ndugu. 9Msimuite mtu yeyote hapa duniani kuwa baba yenu, kwa kuwa mnaye Baba mmoja tu, naye yuko mbinguni. 10Wala msije kuitwa 'walimu,' kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja tu, yaani Kristo. 11Bali aliye mkubwa miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu. 12Yeyote ajiinuae atashushwa. Na yeyote anaye jishusha atainuliwa.
Watakatifu wa siku
- Mt. Polikarpo, askofu na shahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki