Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 22 Februari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 9 Februari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 22 Februari 2027
Jumatatu · Wiki ya Mtoza Ushuru na Farisayo · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Kufungwa kwa Sikukuu ya Kuingia kwa Bwana Hekaluni
Wiki isiyo na mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
20Tambueni haya ya kwamba, hakuna unabii unaoandikwa kwa sababu ya kujifikirisha kwa nabii mwenyewe. 21Kwa kuwa hakuna unabii uliokuja kwa mapenzi ya mwanadamu, isipokuwa wanadamu waliwezeshwa na Roho Mtakatifu aliyeongea toka kwa Mungu. 2:1Manabii wa uongo walijitokeza kwa Waisraeli, na walimu wa uongo watakuja pia kwenu. Kwa siri wataleta mafundisho ya uongo nao watamkana Bwana aliyewanunua. Wanajiletea uharibifu wa haraka juu yao wenyewe. 2Wengi watafuata njia zao za aibu na kupitia wao wataikufuru njia ya ukweli. 3Kwa uchoyo watawanyonya watu wakitumia maneno ya uongo Hukumu yao haitachelewa, uharibifu utawafuata. 4Maana Mungu hakuwaacha malaika waliokengeuka. Bali aliwatupa kuzimu ili wafungwe minyororo mpaka hukumu itakapowajilia. 5Wala Mungu hakuuvumilia ulimwengu wa zamani. Bali, alimhifadhi Nuhu, mwenye wito wa haki, pamoja na wengine saba, wakati alipoachila gharika juu ya ulimwengu ulioasi. 6Mungu aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kiasi cha kuwa majivu na uharibifu ili iwe mfano kwa ajili ya waovu katika siku za usoni 7Lakini alipofanya hilo, alimwokoa Lutu mtu wa haki, aliyekuwa amehuzunishwa na tabia chafu za wasiofuata sheria za Mungu. 8Kwa kuwa huyo mtu wa haki, aliyeishi nao siku kwa siku akiitesa nafsi yake kwa ajili ya yale aliyoyasikia na kuyaona. 9Kwa hiyo Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wake wakati wa mateso na jinsi ya kuwavumilia waovu kwa ajili ya hukumu katika siku ya mwisho.
Injili
9Iweni macho. Watawapeleka hadi mabarazani, na mtapingwa katika masinagogi. Mtasimamishwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kama ushuhuda kwao. 10Lakini injili lazima kwanza ihubiriwe kwa mataifa yote. 11Watakapo wakamata na kuwakabidhi, msiogope kuhusu kile mtakachosema. Ndani ya muda huo, mtapewa nini cha kusema; hamtakuwa ninyi mtakaoongea, bali Roho Mtakatifu. 12Ndugu atamshitaki ndugu kuuawa, baba na mtoto wake. Watoto watasimama kinyume cha baba zao na kuwasababisha kuuawa. 13Mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, mtu huyo ataokoka.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Nikeforo, wa Antiokia ya Shamu (karibu 257)
- Kupatikana kwa masalia ya Askofu Mtakatifu Inokenti, Askofu wa Irkutsk (1805)
- Mfiadini wa Kikasisi Basili, padri (1930)
- Mfiadini wa Kikasisi Yohana, padri (1938)
- Wafiadini wa Kikasisi Markelo, Askofu wa Sisilia, Filagrio, Askofu wa Kipro, na Pankratio, Askofu wa Tauromenio (karne ya 1)
- Mtakatifu Mtawa Pankratio wa Mapango ya Kyiv, katika Mapango ya Mbali (karne ya 13)
- Watakatifu Watawa Genadi (karibu 1516) na Nikeforo (1557) wa Ziwa Vazha
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 9 Februari katika kalenda ya kanisa ni 22 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki