Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 29 Januari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 29 Januari 2027

Ijumaa · Juma la 3 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 3 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ebr 10:32–39

32Lakini kumbuka siku zilizopita, baada ya kutiwa kwenu nuru, ni jinsi gani mliweza kuvumilia maumivu makali. 33Mlikuwa mmewekwa wazi katika dhihaka ya matukano na mateso, na mlikuwa washiriki pamoja na wale waliopitia mateso kama hayo. 34Kwa kuwa mlikuwa na moyo wa huruma kwa hao waliokuwa wafungwa, na mlipokea kwa furaha adhabu ya urithi wenu, mkijua kwamba ninyi wenyewe mlikuwa na urithi bora na wa kudumu milele. 35Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, ulio na zawadi kuu. 36Kwa kuwa mnahitaji uvumilivu, ili kwamba mpate kupokea ambacho Mungu amekiahidi, baada ya kuwa mmekwisha yatenda mapenzi yake. 37Kwa kuwa baada ya kitambo kidogo, mmoja anayekuja, atakuja hakika na hatakawia. 38Mwenye haki wangu ataishi kwa imani. Kama atarudi nyuma, sitapendezwa naye.” 39Lakini sisi si kama wale warudio nyuma kwa kuangamia. Badala yake, sisi ni baadhi ya wale tulio na imani ya kuzilinda roho zetu.

Wimbo wa katikati

Zab 37:3–6, 23–24, 39–40

3Uwamini Mungu na kufanya yaliyo mema; uishi katika nchi na uongezeke katika imani. 4Kisha ufurahi mwenyewe katika Yahwe, naye atakupa matamanio ya moyo wako. 5Umkabidhi njia zako Yahwe; uamini katika yeye, naye atatenda kwa niaba yako. 6Yeye ataidhihilisha haki yako kama mchana na usafi wako kama mwangaza wa mchana. 23Hatua za mwanadamu zinaimarishwa na Yahwe, mtu ambaye njia zake zinakubalika machoni pa Mungu. 24Ajapojikwaa, hataanguka chini, kwa kuwa Yahwe anamshikilia kwa mkono wake. 39Wokovu wa haki unatoka kwa Yahwe; yeye huwalinda wao nyakati za shida. 40Yahwe huwasaidia na kuwaokoa. Yeye huwaokoa dhidi ya watu waovu na kuwanusuru wao kwa sababu wao wamemkimbilia yeye kwa ajili ya usalama.

Injili

Mk 4:26–34

26Na akasema, “Ufalme wa Mungu umefananishwa na mtu aliyepanda mbegu katika udongo. 27Alipolala usiku na kuamka asubuhi, na mbegu zikachipuka na kukua, ingawa hajui ilivyotokea. 28Dunia hutoa mbegu yenyewe; kwanza majani, halafu maua, halafu mbegu zilizo komaa. 29Na wakati mbegu itakapokua imeiva mara hupeleka mundu, kwa sababu mavuno yamewadia.” 30Na akasema, “tuufananishe ufalme wa Mungu na kitu gani, au tutumie mfano gani kuuelezea?. 31Ni kama mbegu ya haradali, ambapo ilipopandwa ni ndogo sana kuliko mbegu zote duniani. 32Hata, wakati imepandwa, inakuana kuwa kubwa zaidi ya mimea yote ya bustani, na inafanya matawi makubwa, hata ndege wa mbinguni huweza kufanya viota vyao kwenye kivuli chake.” 33Kwa mifano mingi alifundisha na alisema neno kwao, kwa kadiri walivyoweza kuelewa, 34na hakusema nao bila mifano. Lakini wakati alipokuwa peke yake, akawaelezea kila kitu wanafunzi wake.

Watakatifu wa 29 Januari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki