Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 22 Januari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 22 Januari 2027

Ijumaa · Juma la 2 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 2 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Vinsenti, shemasi na shahidi · Kumbukumbu ya hiari

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ebr 8:6–13

6Lakini sasa Kristo amepokea huduma bora zaidi kwa sababu yeye pia ni mpatanishi wa agano zuri, ambalo limekwisha kuimarishwa kwa ahadi nzuri. 7Hivyo kama agano la kwanza lisingekuwa na makosa, ndipo hakungekuwa na haja kutafuta agano la pili. 8Kwa kuwa wakati Mungu alipogundua makosa kwa watu alisema, “Tazama, siku zinakuja, 'asema Bwana, 'wakati nitakapotengeneza agano jipya pamoja na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 9Halitakuwa kama agano nililofanya pamoja na baba zao siku ambayo niliwachukua kwa mkono kuwaongoza kutoka nchi ya Misri. Kwa kuwa hawakuendelea katika agano langu, nami sikuwajali tena,' asema Bwana. 10Kwa kuwa hili ndilo agano nitafanya kwa nyumba ya Israeli baada ya siku hizo,' asema Bwana. 'nitaweka sheria zangu mawazoni mwao, na nitaziandika mioyoni mwao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 11Hawatafundishana kila mmoja na jirani yake, na kila mmoja na ndugu, yake, akisema, “Mjue Bwana,” hivyo wote watanijua mimi, kutoka mdogo hadi mkubwa wao. 12Hivyo nitaonyesha rehema kwa matendo yao yasiyo ya haki, na sizitazikumbuka dhambi zao tena.” 13Kwa kusema “Mpya,” amelifanya agano la kwanza kuwa kuukuu. Na hilo ambalo amelitangaza kuwa kuukuu liko tayari kutoweka.

Wimbo wa katikati

Zab 85:7, 9–13

7Utuoneshe sisi uaminifu wa agano lako, Yahwe, utupe sisi wokovu wako. 9Hakika wokovu wake u karibu na wale wanao mwabudu yeye; kisha utukufu utabaki katika nchi yetu. 10Uaminifu wa agano na uaminifu vimekutana pamoja; haki na amani vimebusiana. 11Uaminifu unatoa chemchem kutoka ardhini, na haki hutazama chini kutoka mawinguni. 12Ndiyo, Yahwe atatoa baraka zake njema, na nchi itatoa mazao yake. 13Haki itaenda mbele zake na kufanya njia kwa ajili ya nyayo zake.

Injili

Mk 3:13–19

13Alienda juu ya mlima, na akawaita aliowataka, na wakaenda kwake. 14Akawachagua kumi na wawili (aliowaita mitume), ili kwamba wawe pamoja naye na aweze kuwatuma kuhubiri, 15na kuwa na mamlaka ya kutoa mapepo. 16Na akawachagua kumi na wawili: Simoni, aliyempa jina la Petro, 17Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, aliyepewa jina la Bonagesi, hao ni, wana wa ngurumo, 18na Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo, 19na Yuda Iskariote, ambaye atamsaliti.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 22 Januari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki