Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 13 Januari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 13 Januari 2027

Jumatano · Juma la 1 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 1 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Hilari wa Poitiers, askofu na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ebr 2:14–18

14Kwa hiyo, kwa kuwa watoto wa Mungu wote hushiriki mwili na damu, kadhalika Yesu alishiriki vitu vilevile, ili kwamba kupitia kifo apate kumdhohofisha yule ambaye ana mamlaka juu ya mauti, ambaye ni ibilisi. 15Hii ilikuwa hivyo ili awaweke huru wale wote ambao kupitia hofu ya kifo waliishi maisha yao yote katika utumwa. 16Kwa hakika siyo malaika anaowasaidia. Badala yake, anawasaidia wazao wa Abraham. 17Kwa hiyo, ilikuwa lazima yeye awe kama ndugu zake katika njia zote, ili aweze kuwa kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu kwa vitu vya Mungu, na ili kwamba awe na uwezo wa kutoa msamaha kwa dhambi za watu. 18Kwa sababu Yesu mwenyewe ameteseka, na kujaribiwa, ana uwezo wa kuwasaidia wale wanaojaribiwa.

Wimbo wa katikati

Zab 105:1–4, 6–9

1Mshukuruni Yahwe, liitieni jina lake; myafanye matendo yake yajulikane kati ya mataifa. 2Mwimbieni yeye, mwimbieni sifa yeye; semeni matendo yake yote ya ajau. 3Mjivune katika utakatifu wa jina lake; moyo wao wamtafutao Yahwe ufurahi. 4Mtafuteni Yahwe na nguvu zake; utafuteni uwepo wake siku zote. 6miujiza yake na amri zitokazo kinywani mwake, enyi kizazi cha Ibrahimu mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wachaguliwa wake. 7Yeye ni Yahwe, Mungu wetu. Amri zake ziko juu ya nchi yote. 8Naye hulikumbuka agano lake milele, neno alilo amuru kwa ajili ya vizazi elfu. 9Hulikumbuka agano alilolifanya na Ibrahimu na kiapo alicho mwapia Isaka.

Injili

Mk 1:29–39

29Na mara moja baada ya kutoka nje ya sinagogi, waliingia nyumbani mwa Simoni na Andrea wakiwa na Yakobo na Yohana. 30Sasa mama mkwe wa Simoni alikuwa amelala mgonjwa wa homa, na mara moja walimwambia Yesu habari zake. 31Hivyo alikuja, alimshika kwa mkono, na kumwinua juu; homa ikaondoka kwake, na akaanza kuwahudumia. 32Jioni hiyo wakati jua limekwisha zama, walimletea kwake wote waliokuwa wagonjwa, au waliopagawa na pepo. 33Mji wote walikusanyika pamoja katika mlango. 34Aliwaponya wengi waliokuwa wagonjwa wa magonjwa mbalimbali na kutoa pepo wengi, bali hakuruhusu pepo kuongea kwa sababu walimjua. 35Aliamka asubuhi na mapema, wakati ilikuwa bado giza; aliondoka na kwenda mahali pa faragha na aliomba huko. 36Simoni na wote waliokuwa pamoja naye walimtafuta. 37Walimpata na wakamwambia, “Kila mmoja anakutafuta” 38Aliwaambia, “Twendeni mahali pengine, nje katika miji inayozunguka, ili niweze kuhubiri huko pia. Ndiyo sababu nilikuja hapa.” 39Alikwenda akipita Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kukemea pepo.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 13 Januari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki