Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 14 Januari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 14 Januari 2027
Alhamisi · Juma la 1 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Alhamisi ya Juma la 1 la Mwaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
7Kwa hiyo, ni kama Roho Mtakatifu asemavyo, “Leo, kama utasikia sauti yake, 8Usiufanye moyo wako kuwa mgumu kama Waisraeli walivyofanya katika uasi, katika wakati wa kujaribiwa nyikani. 9Huu ulikuwa wakati ambao baba zenu waliniasi kwa kunijaribu, na wakati, kwa miaka arobaini, waliona matendo yangu. 10Kwa hiyo sikufurahishwa na kizazi hicho. Nilisema, 'Wanapotea kila mara katika mioyo yao, na hawajui njia zangu. 11Ni kama vile nilivyoapa katika hasira yangu: hawataiingia raha yangu.” 12Muwe waangalifu, ndugu, ili kwamba usije ukawepo moyo mwovu wa kutokuamini kwa mmoja wenu, moyo ambao utakwenda mbali na Mungu aliye hai. 13Badala yake, mhamasishane kila siku kila mmoja na mwenzie, ili kila iitwapo leo mtamani, ili kwamba mmoja kati yenu asifanywe kuwa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 14Kwa maana tumekuwa washiriki wa Kristo ikiwa tutashikamana na uthabiti wetu kwa nguvu katika yeye kutoka mwanzo hadi mwisho.
Wimbo wa katikati
6Oh njoni, tumwabudu na tupige magoti; tupige magoti mbele za Yahwe, muumbaji wetu: 7Kwa maana yeye ni Mungu wetu, na sisi tu watu wa malisho yake na kondoo wa mkono wake. Ni heri leo mngesikia sauti yake! 8Msiifanye migumu mioyo yenu, kama vile huko Meriba, au kama ile siku ya Masa jangwani, 9ambako baba zenu walinijaribu na kunipima, japo walikuwa wameyaona matendo yangu. 10Kwa miaka arobaini nilikasirishwa na kizazi hicho na kusema, 'Hawa ni watu ambao mioyo yao imepotoka; hawazijui njia zangu.' 11Hivyo katika hasira yangu niliapa kwamba wasingeingia kamwe mahali pa pumziko.”
Injili
40Mwenye ukoma mmoja alikuja kwake. Alikuwa akimsihi; alipiga magoti na alimwambia, “Kama unataka, waweza kunifanya niwe safi.” 41Akisukumwa na huruma, Yesu alinyosha mkono wake na kumgusa, akimwambia, “Ninataka. Uwe msafi.” 42Mara moja ukoma ukamtoka, na alifanywa kuwa safi. 43Yesu akamwonya vikali na akamwambia aende mara moja, 44Alimwambia, “Hakikisha hausemi neno kwa yeyote, lakini nenda, ujionyeshe kwa kuhani, na utoe dhabihu kwa ajili ya utakaso ambayo Musa aliagiza, kama ushuhuda kwao.” 45Lakini alikwenda na kuanza kumwambia kila mmoja na kueneza neno zaidi hata Yesu hakuweza tena kuingia mjini kwa uhuru. Hivyo alikaa mahali pa faragha na watu walikuja kwake kutoka kila mahali.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki