Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 13 Januari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 31 Desemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 13 Januari 2027
Jumatano · Wiki ya 33 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Kufungwa kwa Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Kristo
Siku za Noeli (Sviatki)
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
9Jitahidi kuja kwagu haraka. 10Kwa kuwa Dema ameniacha. Anaupenda ulimwengu wa sasa na amekwenda Thesalonike, Kreseni alikwenda Galatia, na Tito alikwenda Dalmatia. 11Luka tu ndiye yuko pamoja nami. Umchukue Marko uje naye kwani yeye ni muhimu kwangu katika huduma. 12Nimemtuma Tikiko Efeso. 13Lile joho ambalo nililiacha Troa kwa Karpo, utakapokuja lilete, pamoja na vile vitabu hasa vile vya ngozi. 14Alekizanda mfua chuma alinitendea maovu mengi. Bwana atamlipa kulingana na matendo yake. 15Nawe pia jihadhari naye, kwani aliyapinga sana maneno yetu. 16Katika utetezi wangu wa kwanza, hakuna mtu yeyote aliyesimama pamoja nami, badala yake, kila mmoja aliniacha. Mungu asiwahesabie hatia. 17Lakini Bwana alisimama pamoja nami, akanitia nguvu ili kwamba kupitia kwangu, neno linenwe kwa ukamilifu na mataifa wapate kusikia. Niliokolewa katika kinywa cha Simba. 18Bwana ataniepusha na matendo yote maovu na kuniokoa kwa ajili ya ufalme wake wa mbinguni. Utukufu uwe kwake milele na milele. Amen 19Msalimie Priska, Akila na nyumba ya Onesiforo. 20Erasto alibaki huko Korintho, lakini Trifimo nilimuacha Mileto akiwa mgonjwa. 21Fanya hima uje kabla ya kipindi cha baridi. Eubulo anakusalimu, pia Pude, Lino, Claudia na ndugu wote. 22Mungu awe pamoja na roho yako, Neema iwe nawe.
Injili
23Amini nawaambia kwamba kila auambiaye mlima huu, 'Ondoka, na ukajitupe mwenyewe baharini, 'na kama hana mashaka moyoni mwake lakini anaamini kwamba alichokisema kitatokea, hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya. 24Kwa hiyo ninawaambia: kila kitu muombacho na kuuliza kwa ajili yake, aminini kwamba mmepokea, navyo vitakuwa vyenu. 25Wakati mnaposimama na kuomba, mnapaswa kusamehe chochote mlichonacho dhidi ya yeyote, ili kwamba Baba yenu aliye mbinguni awasamehe pia ninyi makosa yenu.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Melania Mroma (439)
- Askofu Mtakatifu Petro Mohyla, Mitropoliti wa Kyiv (1646)
- Mtakatifu Dositheo Mwungamaji, Mitropoliti wa Zagreb (1945)
- Mfiadini wa Kikasisi Mikaeli, padri (1937)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 31 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 13 Januari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki