Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 12 Januari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 12 Januari 2027

Jumanne · Juma la 1 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumanne ya Juma la 1 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ebr 2:5–12

5Mungu hakuuweka ulimwengu ujao, ambao tunaongelea habari zake, chini ya malaika. 6Badala yake, mtu fulani ameshuhudia mahali fulani akisema, “Mtu ni nani, hata uweze kumkumbuka? Au mwana wa mtu, hata umtunze? 7mtu kuwa mdogo kuliko malaika; umemvika taji ya utukufu na heshima. 8Umeweka kila kitu chini ya miguu yake.” Kwa hiyo Mungu ameweka kila kitu chini ya mtu. Hakuacha kitu chochote ambacho hakiko chini yake. Lakini sasa hivi hatuoni bado kila kitu kikiwa chini yake. 9Hata hivyo, tunaona ambaye alikuwa amefanywa kwa muda, chini kuliko malaika—Yesu, ambaye, kwa sababu ya mateso yake na kifo chake, amevikwa taji ya utukufu na heshima. Hivyo sasa kwa neema ya Mungu, Yesu ameonja kifo kwa ajili ya kila mtu. 10Ilikuwa sahihi kwamba Mungu, kwa sababu kila kitu kipo kwa ajili yake na kupitia yeye, alipaswa kuwaleta watoto wengi katika utukufu, na kwamba alipaswa kumfanya kiongozi katika wokovu wao kuwa mkamilifu kupitia mateso yake. 11Kwa maana wote wawili yule anayeweka wakfu na wale ambao wanawekwa wakfu, wote wanatoka kwenye asili moja, Mungu. Kwa sababu hii yule anayewaweka wakfu kwa Mungu haoni aibu kuwaita ndugu. 12Anasema, “Nitatangaza jina lako kwa ndugu zangu, nitaimba kuhusu wewe kutoka ndani ya kusanyiko.”

Wimbo wa katikati

Zab 8:1, 4–8

1Kwa kiongozi wa muziki; weka kwenye mtindo wa gittith. Zaburi ya Daudi. Yahweh Bwana wetu, ni jinsi gani jina lako ni tukufu katika dunia yote, wewe ufunuaye utukufu wako juu mbinguni. 4Binadamu ni nani hata umtazame, na watu hata uwajali wao? 5Umewaumba chini kidogo kuliko viumbe vya mbinguni na umewazunguka na utukufu na heshima. 6Umemfanya binadamu kutawala kazi ya mikono yako; umeviweka vitu vyote chini ya miguu yake: 7kondoo na ng'ombe wote, na hata wanyama wa porini, 8ndege wa angani, na samaki wa baharini, na vyote vipitavyo katika mikondo ya bahari.

Injili

Mk 1:21–28

21Na walipofika Kaperinaumu, siku ya Sabato, Yesu aliingia kwenye sinagogi na kufundisha. 22Walilishangaa fundisho lake, kwa vile alikuwa akiwafundisha kama mtu ambaye ana mamlaka na siyo kama waandishi. 23Wakati huo huo kulikuwa na mtu katika sinagogi lao aliyekuwa na roho mchafu, na alipiga kelele, 24akisema, “Tuna nini cha kufanya na wewe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani. Wewe ni Mtakatifu pekee wa Mungu!” 25Yesu alimkemea pepo na kusema, “Nyamaza na utoke ndani yake!” 26Na roho mchafu alimwangusha chini na akatoka kwake wakati akilia kwa sauti ya juu. 27Na watu wote walishangaa, hivyo wakaulizana kila mmoja, “Hii ni nini? Fundisho jipya lenye mamlaka? Hata huamuru pepo wachafu nao wanamtii!” 28Na habari kuhusu yeye mara moja zikasambaa kila mahali ndani ya mkoa wote wa Galilaya.

Watakatifu wa 12 Januari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki