Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 9 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 9 Desemba 2026
Jumatano · Juma la 2 la Majilio
Sikukuu na watakatifu
Jumatano ya Juma la 2 la Majilio
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: zambarau
Mt. Yohane Diego · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
25Ni nani tena utakayemfananisha na mimi, ni nani ninayefanan nae?'' amesema mtakatifu. 26Tazama juu kwenye anga! Nani aliyeziumba nyota hizi zote? Analileta nje jeshi na anawaita kwa majina yote. Kwa ukuu wa nguvu zake na kwa uimara wa nguvu zake, hakuna hata mmoja atakayekosa. 27Kwa nini unasema, Yakobo, na kutangaza, Israeli, ''Njia yangu imefichwa Yahwe asione, na Mungu wangu hakuwekwa wazi kuhusiana na uthibitisho wangu''? 28Je hakufahamu? Mungu wa milele, Yahwe, Muumbaji wa miisho ya nchi, apatwi na uchovu wala hachoki; hakuna mipaka katika ufahamu wake. 29Anawapa nguvu waliochoka; na atawapa nguvu mpya waliowadhaifu. 30Hata vijana wadogo watapatwa na uchovu na kuchoka, vijana wadogo watapata mashaka na kuanguka: 31Lakini wale watakao mngojea Yahwe watapewa nguvu mpya; na watapaa kwa mbawa kama malaika; watakimbia wala hawatachoka; watatembea wala hawatazimia.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi. Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote, na vyote vilivyomo ndani yangu, nitalisifu jina lake takatifu. 2Maishani mwangu mwote nitamsifu Yahwe, na kukumbuka matendo yake yote mazuri. 3Yeye husamehe dhambi zako zote; huponya magonjwa yako yote. 4Huukomboa uhai wako dhidi ya uharubifu; hukuvika taji kwa uaminifu wa agano lake na hutenda kwa rehema. 8Yahwe ni wa huruma na neema; ni mvumilivu; ana agano kuu la uaminifu. 10Hatushughulikii sisi kama dhambi zetu zinavyostahili au kutulipa kulingana na uhitaji wa dhambi zetu.
Injili
28Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. 29Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. 30Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
Watakatifu wa siku
- Mt. Yohane Diego
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki