Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 9 Desemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 26 Novemba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 9 Desemba 2026

Jumatano · Wiki ya 28 baada ya Pentekoste · Sauti ya 2

Sikukuu na watakatifu

Mtakatifu Mtawa Alipio, mkaa nguzoni (640)

Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana

Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

2 Tim 4:9–22

9Jitahidi kuja kwagu haraka. 10Kwa kuwa Dema ameniacha. Anaupenda ulimwengu wa sasa na amekwenda Thesalonike, Kreseni alikwenda Galatia, na Tito alikwenda Dalmatia. 11Luka tu ndiye yuko pamoja nami. Umchukue Marko uje naye kwani yeye ni muhimu kwangu katika huduma. 12Nimemtuma Tikiko Efeso. 13Lile joho ambalo nililiacha Troa kwa Karpo, utakapokuja lilete, pamoja na vile vitabu hasa vile vya ngozi. 14Alekizanda mfua chuma alinitendea maovu mengi. Bwana atamlipa kulingana na matendo yake. 15Nawe pia jihadhari naye, kwani aliyapinga sana maneno yetu. 16Katika utetezi wangu wa kwanza, hakuna mtu yeyote aliyesimama pamoja nami, badala yake, kila mmoja aliniacha. Mungu asiwahesabie hatia. 17Lakini Bwana alisimama pamoja nami, akanitia nguvu ili kwamba kupitia kwangu, neno linenwe kwa ukamilifu na mataifa wapate kusikia. Niliokolewa katika kinywa cha Simba. 18Bwana ataniepusha na matendo yote maovu na kuniokoa kwa ajili ya ufalme wake wa mbinguni. Utukufu uwe kwake milele na milele. Amen 19Msalimie Priska, Akila na nyumba ya Onesiforo. 20Erasto alibaki huko Korintho, lakini Trifimo nilimuacha Mileto akiwa mgonjwa. 21Fanya hima uje kabla ya kipindi cha baridi. Eubulo anakusalimu, pia Pude, Lino, Claudia na ndugu wote. 22Mungu awe pamoja na roho yako, Neema iwe nawe.

Injili

Lk 18:15–17, 26–30

15Watu walimletea watoto wao wachanga, ili aweze kuwagusa, lakini wanafunzi wake walipoona hayo, wakawazuia. 16Lakini Yesu akawaita kwake akisema, 'Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie. Maana ufalme wa Mungu ni wa watu kama hao. 17Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto ni dhahiri hatauingia. ' 26Wale waliosikia hayo, wakasema, 'Nani basi, atakayeweza kuokolewa?' 27Yesu akajibu, 'Mambo yasiyowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu yanawezekana.” 28Petro akasema, 'Naam, sisi tumeacha kila kitu na tumekufuata wewe. ' 29Kisha Yesu akawaambia, Amin, nawaambia kwamba hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto, kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, 30ambaye hatapokea mengi zaidi katika ulimwengu huu, na katika ulimwengu ujao, uzima wa milele. '

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 9 Desemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 26 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 9 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki