Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 23 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 10 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 23 Novemba 2026
Jumatatu · Wiki ya 26 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Mitume Erasto, Olimpa, Herodioni, Sosipatro, Kwarto na Tertio, wa Mitume 70 (karne ya 1)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Paulo, Mtume wa Kristo Yesu, kulingana na amri ya Mungu na Mwokozi wetu Yesu Kristo aliye ujasiri wetu, 2kwa Timotheo mwanangu wa kweli katika imani: Neema, rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu. 3Kama nilivyokusihi nilipoondoka kwenda Makedonia, ubaki Efeso ili kwamba uweze kuwaamru watu fulani wasifundishe mafundisho tofauti. 4Pia wasisikilize hadithi na orodha za nasaba zisizo na mwisho. Haya husababisha mabishano zaidi kuliko kuwasaidia kuendeleza mpango wa Mungu wa imani. 5Basi lengo la agizo hili ni upendo utokao katika moyo safi, katika dhamiri nzuri na katika imani ya kweli. 6Baadhi ya watu wamelikosa lengo wakayaacha mafundisho haya na kugeukia mazungumzo ya kipumbavu. 7Wanataka kuwa waalimu wa sheria, lakini hawafahamu wanachosema au wanachosisitiza.
Injili
13Mtu mmoja katika kusanyiko akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie sehemu ya uruthi wangu.” 14Yesu akamjibu, ni nani aliye niweka kuwa mwamuzi na mpatanishi kati yenu.? 15Ndipo akawaambia, Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo.” 22Yesu akawaambia wanafunzi wake, Kwa hiyo nawaambia msihofu juu ya maisha yenu—ya kuwa mtakula nini au juu ya miili yenu—ya kuwa mtavaa nini 23Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi. 24Angalieni ndege wa angani, hawalimi wala hawavuni. Hawana chumba wala ghala ya kuhifadhia, lakini Baba yenu huwalisha. Ninyi si bora zaidi kuliko ndege! 25Ni yupi kati yenu ambaye akijisumbua ataweza kuongeza dhiraa moja katika maisha yake? 26Ikiwa basi hamuwezi kufanya hicho kitu kidogo kilicho rahisi kwa nini basi kusumbukia hayo mengine?. 27Angalieni maua -yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya, 28Kama Mungu huyavika vizuri majani ya kondeni, ambayo leo yapo, na kesho hutupwa kwenye moto. Je si zaidi atawavika ninyi? enyi wa imani haba! 29Msisumbukie juu ya kuwa mtakula nini au mtakunywa nini, wala msiwe na hofu. 30Kwa kuwa Mataifa yote ya dunia husumbukia mambao yao. Na Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo. 31Lakini tafuteni ufalme wake kwanza, na hayo mengine mtazidishiwa,
Watakatifu wa siku
- Mtawa Mfiadini Nifonti na Mfiadini Aleksanda (1931)
- Wafiadini wa Kikasisi Prokopio, Askofu Mkuu wa Odesa, Dionisio, Yohana na Petro, mapadri (1937)
- Wafiadini wa Kikasisi Augustino, Askofu Mkuu wa Kaluga, na pamoja naye Yohana, padri, Watawa Wafiadini Yoanikio na Serafim, Wafiadini Aleksi, Apolo na Mikaeli (1937)
- Mfiadini Nikolao, Mfiadini Ana na Mtakatifu Boris Mwungamaji, shemasi (1930-1940)
- Wafiadini Olga (1941) na Theoktista (1942)
- Kuteswa kwa gurudumu kwa Mfiadini Mkuu Georgi (303)
- Mfiadini Oreste, tabibu (304)
- Mfiadini wa Kikasisi Milio, Askofu wa Uajemi, na wanafunzi wake wawili (341)
- Mfiadini Konstantino, mwana wa mfalme wa Georgia (842)
- Mtakatifu Mtawa Theostirikto wa Simbola
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 10 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 23 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki