Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 20 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 7 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 20 Novemba 2026
Ijumaa · Wiki ya 25 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Wafiadini wa Melitene: Hieroni, Hesikio, Nikandro, Athanasio, Mama, Barakio, Kaliniko, Theageni, Nikoni, Longino, Theodoro, Valerio, Ksanthio, Theodulo, Kalimako, Eugenio, Theodoko, Ostrikio, Epifani, Maksimiano, Dukitio, Klaudiano, Theofilo, Gigantio, Dorotheo, Theodoto, Kastrikio, Aniketa, Themelio, Eutikio, Hilarioni, Diodoto na Amoniti (karne ya 3)
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
6Sasa tunawaagiza, ndugu, katika jina la Bwana Yesu Kristo, kwamba mwepuke kila ndugu ambaye anaishi maisha ya uvivu na siyo kwa kutokana na desturi ambazo mlipokea kutoka kwetu. 7Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ni sawa kwenu kutuiga sisi. Hatukuishi miongoni mwenu kama wale ambao hawakuwa na nidhamu. 8Na hatukula chakula cha mtu yeyote bila kukilipia. Badala yake, tulifanya kazi usiku na mchana kwa kazi ngumu na kwa shida, ili tusiweze kuwa mzigo kwa yeyote katika ninyi. 9Tulifanya hivi si kwa sababu hatuna mamlaka. Badala yake, tulifanya hivi ili tuwe mfano kwenu, ili kwamba mweze kutuiga sisi. 10Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, “Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile.” 11Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi wanaenenda kwa uvivu miongoni mwenu. Hawafanyi kazi lakini badala yake ni watu wasio na utaratibu. 12Sasa hao nao tunaagiza na kuwaasa katika Bwana Yesu Kristo, kwamba lazima wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe. 13Lakini ninyi, ndugu, msizimie roho katika kufanya yaliyo sahihi. 14Ikiwa mtu yeyote hataki kutii neno letu katika waraka huu, mwe makini naye na msiwe na ushirika pamoja naye, ili kwamba aweze kuaibika. 15Msimchukulie kama adui, lakini mwonyeni kama ndugu. 16Bwana wa amani mwenyewe awape amani wakati wowote katika njia zote. Bwana awe nanyi nyote. 17Hii ni salam yangu, Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe, ambayo ni alama katika kila waraka. Hivi ndivyo niandikavyo. 18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iweze kuwa nanyi nyote.
Waraka (ya Jumamosi)
3Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo, 4aliyejitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu ili kwamba atukomboe na nyakati hizi za uovu, kutokana na mapenzi ya Mungu wetu na Baba. 5Kwake uwe utukufu milele na milele. 6Ninashangaa kwamba mnageukia haraka kwenye injili nyingine. Ninashangaa kwamba mnageukia mbali kutoka kwake yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo. 7Hakuna injili nyingine, lakini kuna baadhi ya watu wanao wasababishieni nyinyi matatizo na kutaka kubadilisha injili ya Kristo. 8Lakini hata kama ni sisi au malaika kutoka mbinguni atatangaza kwenu injili tofauti na ile tuliyoitangaza kwenu, na alaaniwe. 9Kama tulivyo sema mwanzoni, na sasa nasema tena, “Kama kuna mtu atawatangazia kwenu injili tofauti na mliyoipokea, na alaaniwe.” 10Kwani sasa hivi ninatafuta uthibitisho wa watu au Mungu? Ninatafuta kuwafurahisha wanadamu? Kama ninaendelea kujaribu kuwafurahisha wanadamu, mimi sio mtumishi wa Kristo.
Injili
2Na hapatakuwepo na siri iliyofichika ambayo haitafunuliwa, wala jambo lililofichwa ambalo halitajulikana. 3Na lolote mlilolisema katika giza, litasikiwa katika mwanga. Na yoyote mliyoyasema kwenye sikio ndani ya vyumba vyenu vya ndani vilivyofungwa yatatangazwa juu ya paa la nyumba. 4Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili na kisha hawana kitu kingine cha kufanya, 5Lakini nitawaonya mtakaye mwogopa. Mwogopeni yule ambaye baada ya kuwa ameua, ana mamlaka ya kutupa jehanamu. Ndiyo, nawaambiani ninyi, mwogopeni huyo. 6Je shomoro watano hawauzwi kwa sarafu mbili? hata hivyo hakuna hata mmoja wao atakayesahaulika mbele za Mungu. 7Lakini mjue kuwa, nywele za vichwa vyenu vimehesabiwa. Msiogope. Ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi. 8Ninawaambia, yeyote atakayenikiri Mimi mbele za watu, Mwana wa Adamu atamkiri mbele za malaika wa Mungu. 9Lakini yeyeyote atakayenikana mbele za watu naye atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu. 10Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa. 11Watakapowapeleka mbele za wakuu wa masinagogi, watawala, na wanye mamlaka, msiogope juu na namna ya kuongea katika kujitetea au nini mtakachosema, 12kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha namna mtakavyosema kwa wakati huo.”
Injili (ya Jumamosi)
1Akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa uwezo na mamlaka juu ya mapepo yote na kuponya magonjwa. 2Akawatuma waende kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 3Akawaambia, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari yenu wala fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala pesa wala msichukue kanzu mbili. 4Nyumba yoyote mtakayo iingia, kaeni humo mpaka mtakapo ondoka mahali hapo. 5Na kwa wale wasio wapokea, mtakapo ondoka mji huo, jikung'uteni vumbi katika miguu yenu kwa ushuhuda juu yao”. 6Wakaondoka na kwenda kupitia vijijini, wakitangaza habari njema na kuponya watu kila mahali.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Lazaro wa Galisio (1053)
- Wafiadini wa Kikasisi Kirilo, Mitropoliti wa Kazan, Mikaeli, Aleksanda, Aleksanda, Mikaeli, Aleksanda, Nikolao, Aleksi, Paulo, Basili, Paulino, mapadri, Yohana na Benyamini, mashemasi, Mfiadini Nikolao, Mfiadini Elisabeti (1937)
- Wafiadini wa Kikasisi Sergio, Askofu Mkuu wa Yelets, Nikolao, padri, na Mfiadini Georgi (1937)
- Wafiadini Melasipo na Kasinia na mwana wao Antonino (363)
- Mtakatifu Mtawa Zosima wa Vorbozomsk (karibu 1550)
- Mtakatifu Mtawa Kirilo wa Novoyezero (1532)
- Wafiadini Aukto, Taurioni na Thesalonikia
- Ikoni ya Mama wa Mungu iitwayo “Kuruka kwa Furaha”, ya Ugresha (1795)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 7 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 20 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki