Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 14 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 1 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 14 Novemba 2026
Jumamosi · Wiki ya 24 baada ya Pentekoste · Sauti ya 6
Sikukuu na watakatifu
Matabibu wasiopokea malipo na watenda miujiza Kosma na Damiani wa Asia na mama yao Mtakatifu Mtawa Theodotia (karne ya 3)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Nahisi kwamba mngevumiliana na mimi katika baadhi ya upumbavu. Lakini kwa kweli mnavumiliana na mimi. 2Kwa kuwa ni mwenye wivu kuhusu ninyi. Nina wivu wa Mungu kwa ajili yenu, tangu nilipowaahidi ninyi kwenye ndoa ya mume mmoja. Niliahidi kuwaleta ninyi kwa Kristo kama bikra safi. 3Lakini ninaogopa kwamba kwa namna fulani, kama nyoka alivyomdanganya Eva kwa hila yake, mawazo yenu yanaweza kupotoshwa mbali kutoka kwenye ibada halisi na safi kwa Kristo. 4Kwa kuwa kwa mfano kwamba mtu fulani akaja na kutangaza Yesu mwingine tofauti na yule tuliyewahubiri. Au kwa mfano kwamba mkapokea roho mwingine tofauti na yule mliyempokea. Au kwa mfano kwamba mkapokea injili nyingine tofauti na ile mliyoipokea. Mkavumilia mambo haya vema inatosha! 5Kwa kuwa nadhani kwamba mimi si miongoni mwa walio duni kwa hao wanaoitwa mitume-bora. 6Lakini hata kama mimi sijafundishwa katika kutoa hotuba, siko hivyo katika maarifa. Kwa kila namna na katika mambo yote tumelifanya hili kujulikana kwenu.
Waraka (Watakatifu Kosma na Damiani)
27Sasa ninyi ni mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. 28Na Mungu ameweka katika kanisa kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu, kisha wale wote watendao matendo makuu, kisha karama za uponyaji, wale wasaidiao, wale wafanyao kazi ya kuongoza, na wote walio na aina mbalimbali za lugha. 29Je sisi sote ni mitume? Sisi sote ni manabii? Sisi sote ni waalimu? Je sisi sote tunafanya matendo ya miujiza? 30Je sisi sote tuna karama ya uponyaji? Sisi sote tunaongea kwa lugha? Sisi sote tunatafsiri lugha? 31Tafuteni sana karama zilizo kuu. Nami nitawaonesha njia iliyo bora zaidi. 13:1Tuseme kwamba ninanena kwa lugha za wanadamu na za malaika. Lakini kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo au upatu uvumao. 2Na kwamba nina karama ya unabii na ufahamu wa kweli zilizofichika na maarifa, na kwamba ninayo imani ya kuhamisha milima. Lakini ikiwa sina upendo, mimi si kitu. 3Na tuseme kwamba ninatoa milki yangu yote na kuwalisha masikini, na kwamba ninautoa mwili wangu ili nichomwe moto. Lakini kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi 5au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya. 6Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli. 7Upendo huvumilia mambo yote; huamini mambo yote, una ujasiri katika mambo yote, na hustahimili mambo yote. 8Upendo haukomi. Ikiwa kuna unabii, wote utapita. Ikiwa kuna lugha, zitakoma. Ikiwa kuna maarifa, yatapita.
Injili
16Sasa, hakuna hata mmoja, anayewasha taa na kuifunika kwa bakuli au kuiweka chini ya kitanda. Badala ya kuiweka kwenye kinara cha taa ili kwamba kila mmoja anayeingia apate kuiona. 17Kwa kuwa hakuna kitakachojificha ambacho hakitajulikana, au chochote kilicho sirini ambacho hakitajulikana kikiwa kwenye mwanga. 18kwa hiyo kuwa makini unapokuwa unasikiliza. Kwa sababu aliye nacho, kwake ataongezewa zaidi, lakini asiye nacho hata kile kidogo alicho nacho kitachukuliwa.” 19baadaye mama yake Yesu na ndugu zake wakaja kwake hawakaribia kwa sababu ya umati wa watu. 20Na akataarifiwa, “Mama yako na ndugu zako wako pale nje wanahitaji kukuona wewe. 21Lakini, Yesu akajibu akasema “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”
Injili (Watakatifu Kosma na Damiani)
1Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili pamoja na kuwapa mamlaka juu ya pepo wachafu, kuwakemea na kuwafukuza na kuponya aina zote za maladhi na aina zote za magonjwa. 5Hawa kumi na wawili Yesu aliwatuma. Naye aliwaelekeza akisema “Msiende sehemu wanakoishi wamataifa na msiingie kwenye miji ya wasamalia. 6Badala yake, mwende kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israel. 7Na mnapokwenda, hubirini na kusema, ufalme wa mbinguni umekaribia.' 8Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma na fukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure.
Watakatifu wa siku
- Wafiadini wa Kikasisi Aleksanda na Theodoro, mapadri (1918)
- Wafiadini wa Kikasisi Aleksanda na Demetrio, mapadri, Mfiadini Elisabeti (1937)
- Mfiadini Petro (1941)
- Wafiadini wa Kikasisi Yohana, askofu, na Yakobo, padri, walioteswa huko Uajemi (karibu 345)
- Wafiadini Kirenia na Yuliana (305-311)
- Mfiadini Hermenegildo, mwana wa mfalme wa Wagothi (586)
- Wafiadini Kaisario, Dasio na wengine watano pamoja nao (karne ya 7)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 1 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 14 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki