Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 14 Novemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 14 Novemba 2026
Jumamosi · Juma la 32 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 32 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Kumbukumbu ya Bikira Maria siku ya Jumamosi · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
5Mpendwa, unaenenda kwa uaminifu unapowahudumia ndugu na wageni, 6ambao wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa. Unafanya vizuri kuwasafirisha katika safari zao kwa namna ambayo inampendeza Mungu. 7Kwa sababu kwa ajili ya Jina, walienda bila kuchukua kitu chochote kutoka kwa watu wa Mataifa. 8Hivyo, tunatakiwa kuwakaribisha watu kama hawa, ili tuwe watenda kazi wenza kwa ajili ya kweli.
Wimbo wa katikati
1Msifuni Yahwe. Amebarikiwa mtu yule anaye mtii Yahwe, apendezwaye sana na amri zake. 2Kizazi chake kitakuwa ni chenye nguvu duniani; kizazi cha mcha Mungu kitabarikiwa. 3Nyumbani mwake mna utajiri na mali; na haki yake itadumu milele. 4Nuru huangazia gizani kwa ajili ya mtu mcha Mungu; yeye ni wa fadhili, huruma, na haki. 5Heri atendaye fadhili na kukopesha, afanyaye mambo yake kwa uaminifu. 6Kwa maana hataondoshwa kamwe; mwenye haki atakumbukwa milele.
Injili
1Kisha akawaambia mfano wa namna wanavyopaswa kuomba daima, na wasikate tamaa. 2akaisema, 'Kulikuwa na hakimu katika mji fulani, ambaye hakuwa anamwogopa Mungu na hakuwaheshimu watu. 3Kulikuwa na mjane katika jiji hilo, naye alimwendea mara nyingi, akisema, 'Nisaidie kupata haki dhidi ya mpinzani wangu.' 4Kwa muda mrefu hakuwa tayari kumsaidia, lakini baada ya muda akasema moyoni mwake, 'Ingawa mimi simwogopi Mungu au kuheshimu mtu, 5lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua nitamsaidia kupata haki yake, ili asije akanichosha kwa kunijia mara kwa mara. '' 6Kisha Bwana akasema, 'Sikiliza alivyosema huyo hakimu dhalimu. 7Je Mungu pia hataleta haki kwa wateule wake ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, yeye hatakuwa mvumilivu kwao? 8Nawaambia kwamba ataleta haki kwao upesi. Lakini wakati Mwana wa Adamu atakapokuja, je, atakuta imani duniani? '
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki