Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 13 Novemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 31 Oktoba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 13 Novemba 2026

Ijumaa · Wiki ya 24 baada ya Pentekoste · Sauti ya 6

Sikukuu na watakatifu

Mitume Stakisi, Ampliato, Urbano, Narkiso, Apele na Aristobulo, wa Mitume 70 (karne ya 1)

Siku ya mfungo

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

1 The 5:9–13, 24–28

9Kwa kuwa Mungu hakutuchagua mwanzo kwa ajili ya gadhabu, bali kwa kupata wokovu kwa njia ya Bwana Yesu Kristo. 10Yeye ndiye aliyetufia ili kwamba, tukiwa macho au tumelala, tutaishi pamoja naye. 11Kwa hiyo, farijianeni na kujengana ninyi kwa ninyi, kama ambavyo tayari mnafanya. 12Ndugu, twawaomba muwatambue wale wanaotumika miongoni mwenu na wale walio juu yenu katika Bwana na wale wanao washauri. 13Tunawaomba pia muwatambue na kuwapa heshima katika upendo kwa sababu ya kazi yao. Muwe na amani miongoni mwenu ninyi wenyewe. 24Yeye aliyewaita ni mwaminifu, naye ndiye mwenye kutenda. 25Ndugu, tuombeeni pia. 26Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu. 27Nawasihi katika Bwana kwamba barua hii isomwe kwa ndugu wote. 28Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.

Injili

Lk 11:23–26

23Yeye asiye pamoja nami yuko kinyume nami, na yeye asiyekusanya pamoja nami hutapanya. 24Pepo mchafu amtokapo mtu, huenda na kutafuta mahali pasipo na maji ili ajipumzishe. Atakapokuwa amekosa, husema, 'nitarudi nilipotoka. 25Akirudi na kukuta nyumba imefagiliwa na imekaa vizuri. 26Hivyo huenda na kutafuta mapepo saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe na kuwaleta waje wakae mahali pale. Na hali ya mtu huyo huwa mbaya kuliko ilivyokuwa mara ya kwanza.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 13 Novemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 31 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 13 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki