Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 3 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 21 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 3 Novemba 2026
Jumanne · Wiki ya 23 baada ya Pentekoste · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Hilarioni Mkuu (371-372)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
6Mlikuwa watu wa kutuiga sisi na Bwana, kama mlivyopokea neno katika taabu kwa furaha itokayo kwa Roho Mtakatifu. 7Na matokeo yake, mkawa mfano kwa wote katika Makedonia na Akaiya ambao wanaamini. 8Kwa kuwa kutoka kwenu neno la Mungu limeenea kote, na si kwa Mekadonia na Akaiya peke yake. Badala yake, kwa kila mahali imani yenu katika Mungu imeenea kote. Na matokeo yake, hatuhitaji kusema chochote. 9Kwa kuwa wao wenyewe wanaarifu ujio wetu ulikuwa wa namna gani kati yenu. Wanasimulia jinsi mulivyomgeukia Mungu kutoka katika sanamu na kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli. 10Walitoa habari kuwa mnamsubiri Mwana wake kutoka mbinguni, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu. Na huyu ni Yesu, anayetuweka huru kutoka kwenye ghadhabu ijayo.
Waraka (ya Jumatano)
1Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua, ndugu, kuwa ujio wetu kwenu haukuwa wa bure. 2Mnajua kwamba mwanzoni tuliteseka na walitutenda kwa aibu kule Filipi, kama mujuavyo. Tulikuwa na ujasiri katika Mungu kunena injili ya Mungu hata katika taabu nyingi. 3Kwa maana mahusia yetu hayatokani na ubaya, wala katika uchafu, wala katika hila. 4Badala yake, kama vile tulivyokubalika na Mungu na kuaminiwa injili, ndivyo tunenavyo. Tunanena, si kwa kuwafurahisha watu, lakini kumfurahisha Mungu. Yeye pekee ndiye achunguzaye mioyo yetu. 5Kwa maana hatukutumia maneno ya kujipendekeza wakati wote wote, kama mjuavyo, wala ukutumia maneno kama kisingizio kwa tamaa, Mungu ni shahidi wetu. 6Wala hatukutafuta utukufu kwa watu, wala kutoka kwenu au kwa wengine. Tungeweza kudai kupendelewa kama mitume wa Kristo. 7Badala yake tulikuwa wapole kati yenu kama mama awafarijivyo watoto wake mwenyewe. 8Kwa njia hii tulikuwa na upendo kwenu. Tulikuwa radhi kuwashirikisha si tu injili ya Mungu bali pia na maisha yetu wenyewe. Kwa kuwa mmekuwa wapendwa wetu.
Waraka (Mt. Hilarioni Mkuu)
6Wazo ni hili: mtu apandaye haba pia atavuna haba, na yeyote apandaye kwa lengo la baraka pia atavuna baraka. 7Basi na kila mmoja atoe kama alivyopanga moyoni mwake. Basi naye asitoe kwa huzuni au kwa kulazimishwa. Kwa kuwa Mungu humpenda yule atoaye kwa furaha. 8Na Mungu anaweza kuizidishia kila baraka kwa ajili yenu, ili kwamba, kila wakati, katika mambo yote, muweze kupata yote mnayohitaji. Hii itakuwa ili kwamba mueze kuzidisha kila tendo jema. 9Ni kama ilivyoandikwa: “Ametapanya utajiri wake na kuutoa kwa maskini. Haki yake yadumu milele.” 10Naye atoaye mbegu kwa mpanzi na mkate kwa ajili ya chakula, pia atatoa na kuzidisha mbegu yenu kwa ajili ya kupanda. Yeye ataongeza mavuno ya haki yenu. 11Mtatajirishwa kwa kila namna ili kwamba muweze kuwa wakarimu. Hii italeta shukrani kwa Mungu kupitia sisi.
Injili
23Akawambia wote, “kama mtu yeyote akitaka kunifuata, lazima ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake kila siku, na anifuate. 24Yeyote ajaribuye kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote apotezae maisha yake kwa faida yangu, atayaokoa. 25Je kitamfaidia nini mwanadamu, kama akiupata ulimwengu wote, lakini akapoteza au akapata hasara ya nafsi yake? 26Yeyote atakaye nionea aibu mimi na maneno yangu, kwake yeye mwana wa Adam atamuonea aibu atakapo kuwa katika utukufu wake, na utukufu wa Baba na malaika watakatifu. 27Lakini ninawaambia ukweli, kuna baadhi yenu wasimamao hapa, hawata onja umauti mpaka wauone ufalme wa Mungu.”
Injili (ya Jumatano)
44“Maneno yawakae masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu atatolewa mikononi mwa wanadamu.” 45Lakni hawakuelewa maana ya maneno hayo, na yalifichwa machoni pao, ili wasije wakalielewa. Waliogopa kumuuliza kuhusu neno hilo. 46Kisha mgogoro ulianza ulizuka miongoni mwao i juu ya nani angekuwa mkuu. 47Lakini Yesu alipotambua walichokuwa wakihojiana mioyoni mwao, alimchukua mtoto mdogo, na kumuweka upande wake, 48na akasema, “ kama mtu yeyote akimpokea mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, anipokea mimi pia, na yeyote akinipokea mimi, ampokea pia aliyenituma, kwa kuwa aliye mdogo kati yenu wote ndiye alie mkuu” 49Yohana akajibu akasema, “Bwana, tulimuona mtu akifukuza pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu haambatani na sisi.” 50Lakini Yesu akamwambia, “Msimzuie, kwa kuwa asiye kinyume na ninyi ni wa kwenu”
Watakatifu wa siku
- Kuhamishwa kwa masalia ya Askofu Mtakatifu Hilarioni, Askofu wa Moglena (1206)
- Wafiadini wa Kikasisi Paulino, Askofu Mkuu wa Mogilev, Arkadio, Askofu wa Yekaterinburg, na pamoja nao Anatoli na Nikandro, mapadri, na Mfiadini Kiprian (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Damiani, Askofu Mkuu wa Kursk (1937)
- Wafiadini wa Kikasisi Konstantino, Sergio, Basili, Theodoro, Vladimir, Nikolao, Yohana, Basili, Aleksanda, Demetrio na Aleksi, mapadri, Sergio na Yohana, mashemasi, na Mtawa Mfiadini Sofronio (1937)
- Mtawa Mfiadini Pelagia (1944)
- Wafiadini Dasio, Gayo na Zotiko (303)
- Mtakatifu Mtawa Silvesta wa Obnora (1379)
- Watakatifu Watawa Theofilo na Yakobo wa Omuch (karibu 1412)
- Mtakatifu Mtawa Hilarioni, mtawa wa skima wa Mapango ya Kyiv (karne ya 11)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 21 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 3 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki